HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 22, 2022

MKUTANO WA TUME YA PAMOJA YA KUDUMU KATI YA TANZANIA, MSUMBIJI WAFANYIKA DAR

 

Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Naimi Aziz akifuatilia utambulisho wa washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022 wakifuatilia mkutano huo wakati wa ufunguzi wake.

Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Faustine Kasike akishiriki katika Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji kutoka nchini Msumbiji akijitambulisha wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022

Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia Tanzania Felix Wandwe akijitambulisha wakati wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji kutoka nchini Msumbiji akijitambulisha wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022


Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Faustine Kasike (wa kwanza kushoto) akiwa na Balozi Naimi Aziz-Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki Balozi Joseph Sokoine wakifuatilia utambulisho wa washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022 wakifuatilia mkutano huo wakati wa ufunguzi wake.



Baadhi ya washiriki wa  Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022 wakifuatilia mkutano huo wakati wa ufunguzi wake.


Mshiriki kutoka Msumbiji katika Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji kutoka nchini Msumbiji akijitambulisha wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022


 

Baadhi ya washiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022 katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano huo.

Baadhi ya washiriki wa Msumbiji katika Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022 katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano huo.

Washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022 katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano huo.

 

Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Msumbiji umeanza leo tarehe 22 Agosti, 2022 katika ngazi ya Wataalamu Jijini Dar es Salaam. 

 

 Mkutano huu wa awali pamoja na mambo mengine utajadili masuala ya ushirikiano yaliyokubaliwa baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Msumbiji. Mkutano huu utafuatiwa na mkutano katika ngazi ya Makatibu Wakuu na ngazi ya Mawaziri utakaofanyika tarehe 24 Agosti, 2022.

 

Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja unalenga kujadili na kutathmini hatua za utekelezaji zilizofikiwa katika masuala mbalimbali ya ushirikiano yaliyokubaliwa kwenye mkutano wa 14 uliofanyika mwaka 2006. 

 

Mkutano huu pia utajadili kuanzisha maeneo mapya ya ushirikiano kwenye sekta za Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maji na Umwagiliaji, Nishati, Madini, Afya, Ujenzi na Uchukuzi, Mifugo, Uvuvi, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Maliasili na Utalii. 

 

Tanzania na Msumbiji zimekuwa zikishirikiana katika maeneo ya Uhusiano wa Kidiplomasia, Ulinzi na Usalama, Fedha, Nishati, Maendeleo ya Jamii, Afya, Kazi, Ujenzi wa Miundombinu, Uchukuzi, Sayansi, Teknolojia, Habari, Elimu,Utamaduni na Sanaa, Biashara na Uwekezaji, Utalii na Wanyamapori, Kilimo, Uvuvi, Maji, Mazingira, Madini, Afya, Mifugo, Nishati na Elimu.

 

Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji ilianzishwa mwaka 1979 na tangu wakati huo jumla ya mikutano 14 imefanyika ambapo maeneo ya ushirikiano yalikuwa yanajadiliwa na kukubaliwa kwa pamoja. Maeneo hayo ni Uhusiano wa Kidiplomasia, Biashara, Mawasiliano, Uchukuzi, Uhamiaji, Ulinzi na Usalama, Kilimo, Utalii na Uvuvi.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki Balozi Joseph Sokoine akifuatilia utambulisho wa washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022 wakifuatilia mkutano huo wakati wa ufunguzi wake.

No comments:

Post a Comment

Pages