Na Victor Masangu
Katika
kuwakomboa vijana ambao wanashindwa kujiendeleza zaidi pindi
wanapomaliza masomo yao ya shule za msingi na sekondari Asasi isiyokuwa
ya kiserikali ya ya Organization for Community Development (OCODE)
imekuja na mpango wa mradi wa pili ujulikanao Kama Bongo lengo ikiwa ni
kuwawezesha vijana.
Mradi
huo ambao kwa Sasa unatekelezwa katika manispaa ya ubungoJijini Dar es
Salaam umeanzishwa maalumu kwa ajili ya kuweza kuwasaidia vijana wenye
kuanzia umri wa miaka 13 hadi 19 ambao walishindwa kuendelea na mfumo
rasmi wa elimu.
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Ocode Joseph Jackson wakati wa
halfa ya mahafali kwa vijana wapatao 193 ambao wameweza kuhitimu baada
ya kumaliza masomo yao kutoka Veta na kufanikiwa kujifunza katika fani
mbali mbali.
Mkurugenzi
huyo alibainisha kuwa lengo la mradi huo ni kuweka mipango madhubuti
ambayo itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa vijana wa manispaa ya ubungo
kuweza kupata fursa ya kujiajiri wao wenyewe na hatimaye kujikwamua
kiuchumi.
"Katika mradi
huu wa bongo tumejikita zaidi kwa vijana na kwamba una malengo makuu
matatu ambayo moja wapo ni kuwapatia watoto fursa ya elimu Bora,lakini
pili ni kuwapa vijana stadi mbali mbali za maisha na jambo lingine la
tatu ni kuwasaidia vijana katika suala zima la kujikwamua kiuchumi ili
wasiwe tegemezi,"alisema Jakson.
Aidha
alibainisha kwamba mradi huo wa bonga kwa sasa ni awamu ya pili na
kwamba vijana hao walioweza kuhitimu wataweza kuleta chachu ya
mabadiliko kutokana na ujuzi na fani mbali mbali ambazo wamezisomea
katika chuo Cha Veta.
Kwa
upande wake mjumbe wa bodi ya Ocode Godfrey Boniventura ambaye
alimwakilisha Mwenyekiti wa bodi hiyo alibainisha kuwa kati ya wahitimu
hao 193 waliomaliza wameweza kujifunza kozi tofauti ikiwemo ushonaji wa
nguo.kupika.kupamba,fani ya kutengeneza simu,udereva pamoja na fani
nyingine.
Aidha mjumbe
huyo aliongeza kwamba katika fani hizo kwa kiasi kikubwa vinagusa maisha
ya watu hivyo ana Imani kubwa vijana hao watakuwa mabalozi wazuri
katika jamii kwa kile ambacho wamefundishwa na kuwasihi wasibweteke na
badala yake waongeze ujuzi na ubunifu zaidi katika kutimiza malengo yao.
Katika
hatua nyingine aliwataka kuachana na tabia ya kukaa katika makundi
ambayo hayana msaada kwao na badala yake waweze kujiunga kwa pamoja kwa
kuongeza thamani ya ujuzi wao ili waweze kupata soko kwa urahisi zaidi.
Naye
Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
mahafali hayo Hassan Mwasha ameipongeza Asasi ya Ocode kwa kuanzisha
mradi huo wa kuwasaidia vijana na kuahidi kushirikiana nayo bega kwa
bega kwa maslahi ya kuwakomboa vijana.
Pia
aliwaasa vijana wote ambao wamebahatika kupata fursa ya mafunzo hayo
kutokuwa na vitendo vya kuzagaa vijiweni na badala yake waweze kujiunga
katika vikundi lengo ikiwa ni kupatiwa fursa ya mikopo ambayo itaweza
kuwasaidia katika kupambana na wimbi la umasikini.
Naibu
Meya huyo pia hakusita kuwakumbushia vijana hao kuhakikisha wanashiriki
kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi ambalo linatarajiwa
kufanyika Agosti 23 mwaka huu kujitokeza kwa wingi ili serikali iweze
kutambua idadi kamili ya wananchi wake.
Asasi
ya Ocode imekuwa ikifanya kazi zake mbali mbali katika Manispaa ya
Ubungo Jijini Dar es Salaam ambapo imekuwa ikitekeleza miradi ya elimu
kwa vijana pamoja na kuboresha maisha ya jamii pamoja na sekta ya
michezo.
No comments:
Post a Comment