HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 31, 2022

Waalikwa walipa heko Kanisa Halisi la Mungu Baba katika sherehe ya kupeleka Matunda Chanzo Halisi

Asilina Abubakar akitoa ushuhuda katika Ibada ya Sherehe ya Kumletea Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake, iliyofayika Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga, jijini Dar es Salaam.

 

Maelfu ya Uzao wa Kanisa Halisi la Mungu Baba kutoka ndani na nje ya Tanzania pamoja na Waalikwa wa dini na madhehebu mbalimbali, Jumapili Agosti 28, 2022 (Lango la 12 Abu,1) walihudhuria kwa kishindo Ibada ya Sherehe ya Kumletea Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake, iliyofayika Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga, jijini Dar es Salaam.

Mwanzoni mwa Ibada ya sherehe hiyo Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo, Baba Halisi, aliwaongoza wote waliohudhuria kufanya kwanza Shukurani (Maombi) ya kumwinua Rais Samia Suluhu Hassan ili Mungu Baba aweze kumlinda, kumpa afya njema na kumwongezea hekima, busara na maarifa ili aendelee kuliongoza vema Taifa.

Mbali ya kumuombea Rais Samia, pia waumini wa Kanisa hilo wakiongowa na Baba Halisi walifanya Shukurani (maombi) kwa ajili ya Sensa ya Watu na Makazi iliyoanza Agosti 23, mwaka huu, ili itekelezwe kwa kiwango ambacho Serikali imekusudia hasa kwa kutambua Sensa ni jambo muhimu kwa maendeleo ya Taifa na Wananchi wote.

Akiendelea na Ibada hiyo, Baba Halisi kwa hekima busara na kwa mpangilio mzuri wa maneno, alifafanua kwanza kwa kirefu sababu ya Kanisa Halisi la Mungu Baba kuandaa Sherehe hiyo yaKumletea Chanzo Halisi Matunda na kutoa mwaliko kwa kila mtu bila kujali dini au dhehebu.

“Hapa bila shaka lipo swali kwamba kwa nini sote tukusanyike kumletea matunda Chanzo Halisi bila kujali dini au dhehebu la yeyote?", Baba Halisi akasema, kisha akalitolea ufafanuzi swali hilo akisema, huku akinukuu maandiko;

"Sababu kubwa ni kutokuwa na tofauti ya behewa la nje na la ndani tena (Ufunuo 11:1-3). Waliotumwa walikuwa hawaruhusiwi kutoka nje ya kuta nne maana iliandikwa hivyo.  Kwa kuwa yupo Chanzo Halisi mwenyewe ndani ya Moyo wa kila anayetenda haki (Isaya 57:15) yeye hazuiliwi kupima chochote. Maana katika Zekaria 14:9, yeye ni mmoja na jina lake ni moja,”akasema Baba Halisi.

Huku baadhi ya Uzao (Waumini) wakinukuu maneo yake kwa kuandika katika  'Note book' zao, Baba aliendelea kutaja sababu nyingine inayosababisha Kumletea Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake ifanyike bila kujali dini wala dhehebu akasema;

"Ni kwamba ile barabara (njia) ya Mwafrika kuabudu na Muashukuru pamoja, tayari (Isaya 19:23-25).  Iliandikwa kuwa itakuwepo barabara itokayo Afrika kwenda hadi Ashuru, yaani Uarabuni ambayo ni lugha safi (Sefania 3:10)",  akasema Baba Halisi kisha akafafanua kwamba  hiyo barabara tayari ni lugha ya Kiswahili ambacho kimeenea kila mahali na kwamaba hiyo ni sababu ya tatu ambayo inayofanya watu wote kumletee Chanzo Halisi matunda ya shamba lake.”

Baba Halisi ametaja sababu nyingine ni Majira ya Simba na Ng’ombe kulisha pamoja akinukuu (Isaya 11:7-9/Isaya 2:4), Majira ya Kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo wa Yohana na kwamba aliyekuwa anamiliki kila kitu ni Ibilisi kwa mujibu wa Luka 4:5-9.

“Sasa kila kitu kimerejea kwa Chanzo Halisi kwa mujibu wa Rumi 11:36. Ilikuwa ni lazima tumletee Chanzo Halisi matunda ya shamba lake maana yeye anamiliki kila kitu kwa sasa na zaidi amewaponya mengi bila kujali dini wala dhehebu.

Sababu nyingine ni kutokuwepo tena na njia mbaya za kupata utajiri. Wakati wa Majira saba ulikuwa huwezi kupata kitu kizuri mpaka utoe kafara kulingana na kitu unachokitafuta.

Sasa kwa Chanzo Halisi hata kama uliua mke au mtoto, Chanzo Halisi amekushika mkono ili yeye ndiye aonekane kwa kila kitu unachofanya. Usiogope tena kwa kujiuliza kuwa nitaanzaje kunyoosha wakati nilishakukosea , unapomtolea matunda leo, njia mbaya ya dunia ambayo ilikuwa na madai kwako haipo tena,” akasema Baba Halisi.

Kuhusu Tanzania, Baba Halisi alisema, kuna mambo mazuri na makubwa yametokea katika Taifa hilo, lakini bado Watanzania hawajamshukuru aliyewafanyia hayo kama inayoelekezwa katika maandiko.

"Tumepata viongozi wema, tuna amani, Uchumi umeimarika, tumepona janga la kimbunga job, tumepona milipuko ya magonjwa kama corona, tumepona njaa, tumepona mgao wa umeme, tumepona ukame, tumepona jangwa, tumepona maandamano ya vurugu mitaani, tumepona volcano, Taifa tumevuka, na kadhalika.

Kwa haya machache na mengine mengi ni vema wote bila kujali kusanyiko la dini au dhehebu la yeyote, kukutana kama hivi kushukuru aliyetuponya kwa mujibu wa Efeso 4:6, ‘‘kuna Mungu mmoja na Baba wa wote, ambaye yuko juu ya wote, anafanya kazi katika yote na yuko katika yote’’.

Mwishoni mwa Ibada hiyo Baba Halisi aliwashukuru (Uzao) na Makuhani wa Kanisa Halisi la Mungu Baba pamoja na waalikwa wa madhehebu na dini zote, kwa kujumuika kwenye sherehe hiyo ambayo alisema yeye binafsi imemfanya awe mwenye furaha kubwa na anaamini hata wengine nao wamefurahi.

Baba Halisi alieleza kufurahishwa kwake na wote waliohudhuria sherehe hiyo ambapo katika kudhihirisha furaha yake hiyo alitoa zawadi kwa wahudhuraji  mbalimbali akiwemo Kuhani wa Kanisa Halisi Kituo cha Kenya ambaye alimpatia zawadi ya 'CD' ya Ibada ya Jumapili iliyotangulia akisema anampatia zawadi hiyo kwa Kenye kufanya Uchaguzi wake Mkuu kwa Amani na Utulivu.

“Leo nimefurahi sana kwa wote mliohudhuria sherehe hii ya Kumeleta Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake bila kujali dini au dhehebu.”

Matunda aliyopelekewa Cahanzo Halisi kaatika Sherehe hiyo yalikuwa katika mafungu 6, yakiwa ni; Matunda ya Chanzo Halisi, Matunda ya kujenga Moyo, Matunda ya Chanzo cha Sauti, Matunda ya Limbuko, Matunda ya jamii na Matunda ya Shukurani.

Baadhi ya waliohudhuria Sherehe hiyo ni Wakuu wa vyombo vya huduma Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mbweni, Kamishna Msaidizi wa Polisi Ndugu Buchuma ambaye alipokaribisha kuzungumza alisema, amependa yanayofanywa na Kanisa Halisi la Mungu Baba kwa sababu nyingi ikiwemo kuiweka jamii pamoja hasa Vijana.

Alisema, pia analipongeza Kanisa hilo kwa kaulimbiu yake ya 'Ibada ni Uzalishaji' inayohiliza kila mtu kufanyakazi na kaulimbiu ya 'Upendo usiobagua', inayohimiza watu wote kupendana bila kujajali dini au madhehebu yao.


No comments:

Post a Comment

Pages