Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Wizara
ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa Mwaka wa
Fedha 2022/23 imesema kuwa imetenga kiasi cha Sh Bilioni 45 kwa Kundi
wafanyabishara ndogondogo maarufu kama Wamachinga kwa ajili ya
kuendeleza ujenzi wa miundombinu katika masoko na kuwawezesha kupata
mitaji ya kuendeleza biashara zao.
Hayo
yamesemwa leo jijini humo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima wakati akifafanua mbele
ya wanahabari majukumu ya Wizara na utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa
fedha 2022/2023.
Amebainisha
kuwa utekelezaji wa mpango huo unafanyika kwa Ushirikiano baina ya
Wizara za kisekta zikiwemo; Ofisi ya Makamu wa Rais; Ofisi ya Waziri
Mkuu; Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum;
OR-TAMISEMI; Uwekezaji, Viwanda na Biashara; Fedha na Mipango; Mambo ya
Ndani ya Nchi; OR-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na
Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
Amesisitiza
kuwa kuhusu maendeleo ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, Wizara imetenga
Tsh. 5,300,000,000/= kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kujifunzia na
kufundishia katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru na Vyuo nane
vya Maendeleo ya Jamii.
“Fedha
hiyo itatumika kuendelea kujenga na kukarabati mabweni, madarasa, kumbi
za mihadhara, majengo ya utawala pamoja na Maktaba”. Amesema Waziri
Gwajima.
Amesema
katika kuwezesha wanawake kiuchumi, Serikali itaendelea kuhamasisha
wanawake kujiunga katika majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi.
Majukwaa haya yapo kuanzia ngazi ya Kijiji/Mtaa, Kata, Halmashauri, Mkoa
na Ngazi ya Taifa.
“Ili
kuimarisha majukwaa haya, Wizara imepanga kutumia kiasi cha Shilingi
15,940,000 kusambaza Mwongozo wa Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake
Kiuchumi pamoja na kuzindua Jukwaa la Kitaifa la Uwezeshaji Wanawake
Kiuchumi”. Amesema
Ameongeza
kuwa amesema katika kuhakikisha ahadi za nchi zinafikiwa, Serikali iko
katika hatua za mwisho za kukamilisha Andiko linalolenga kuweka
mazingira wezeshi ya utekelezaji wa Ahadi za Nchi kuhusu Jukwaa la
Kizazi Chenye Usawa. Jumla ya Shilingi 81,200,000 imepangwa kutumika.
Ameeleza
kuwa katika kuwezesha wanawake kiuchumi, Serikali itaendelea kutoa
mikopo yenye masharti nafuu kwa wanawake wajasiriamali kupitia Mfuko wa
Maendeleo ya Wanawake ambapo kiasi cha Shilingi 600,000,000 zimetengwa.
“Fedha
hizi ni kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake
wajasiriamali pamoja na mwanamke mjasiriamali mmoja mmoja”. Ameeleza
Waziri Gwajima
Pia
amesema kuwa Serikali itaendelea kuratibu afua za kukuza usawa wa
kijinsia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake. Mwanamke ndiyo mlezi
wa familia na jamii kwa ujumla, hivyo anahitaji kulindwa dhidi ya
vitendo vya ukatili. Katika eneo hili, Wizara imetenga kiasi cha
Shilingi 168,980,000.
No comments:
Post a Comment