Mgombea wa nafasi ya mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji Maryam Sheiban (Twiga).
Na Mwandishi Wetu, Kibaha
Aliyekuwa
mlimbwende namba moja katika kinyang'anyiro cha kumsaka miss Arusha
kwa mwaka 2007 Maryam Sheiban almaarufu (Twiga) amejitosa kuwania
kugombea nafasi ya mjumbe wa halmashauri halmashauri kuu ya chama Cha
mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji.
Mgombea
huyo ambaye kwa sasa amekuwa mstari wa mbele katika kujishighulisha na
mambo mbali mbali ya kijamii katika maeneo ya Kibaha pamoja na Mkoa wa
Pwani kwa ujumla lengo ikiwa ni kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo.
Akizungumza
na waandishi wa habari kuhusiana na uchaguzi huo ambao unatarajiwa
kufanyika mwezi octoba mwaka huu mjini kibaha ameahidi kuleta mapinduzi
ya kimaendeleo kwa kushirikiana na wanachama wenzake wa CCM.
"Lengo
langu kubwa endapo nikifanikiwa kutetea katika nafasi ya mjumbe wa
halmashauri kuu ya CCM katika Wilaya ya Kibaha mji nitaweka mikakati
madhubuti kwa kushirikiana na wenzangu katika kukiimarisha chama katika
kuanzia ngazi ya chini,"alisema Twiga.
Pia
alisema kwamba licha ya kuweka mipango dhabiti ya kukiimarisha chama
pia ataendelea kusimamia na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ili
kuleta mageuzi ya kimaendeleo kwa wananchi wa Kibaha mjini pamoja na
Taifa kwa ujumla.
Mgombea
huyo amesema ana imani endapo atafanikiwa kushinda katika uchaguzi huo
ataendelea kufanya mambo ya kijamii kwa kuwasaidia wananchi kutokana na
mwongozo wa ilani ya chama inavyosema.
Aidha
katika hatua nyingine alipongeza uongozi mzima wa chama Cha mapinduzi
(CCM) katika Wilaya ya Kibaha mji kwa kuweza kushirikiana bega kwa bega
na wanachama katika kufanikisha dhamira ya kukitetea chama na kuwaletea
wananchi maendeleo.
Sambamba
na hilo mgombea huyo alimpongeza kaa dhati Rais wa awamu wa Sita Samia
Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali
mbali ya kimaendeleo ambayo imeweza kuwasaidia wananchi wa Taifa la
Tanzania.
No comments:
Post a Comment