Kuelekea mchezo wa watani wa jadi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC PREMIER LEAGUE) Yanga SC dhidi ya Simba, Ofisa Habari wa Yanga Ally Kamwe amesema wanaenda kuwajibu wanaowabeza kwa vitend.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya Yanga kuondoshwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, maneno yamekuwa mengi kwenye vijiwe vya kidigitali kuhusu ubora wa kikosi cha Wananchi kuporomoka uwezo.
Akizungumzia kauli hizo kupitia kituo cha Radio cha Wasafi FM Ally amesema kuwa hawana muda wa kujibizana na Watu kwaneno bali wanajukumu la kwenda kuonyesha kwa vitendo.
“Kutolewa kwenye Champions League hakuwezi ku-highlight performance ya timu au msimu mzima wa Yanga kwamba ni mbovu.
"Huyu ambaye anatubeza sisi ni wabovu si amesonga mbele? Sisi tumetolewa si wabovu? inshallah jumapili huyu last born mzuri na sisi wabovu pale Benjamin Mkapa baada ya dakika 90 Afrika itafahamu."amesema na kubainisha kuwa.
“Sisi tunataka tukawajibu kwa vitendo, tumeshtushwa na propaganda kwamba Yanga ni mbovu baada ya kutolewa na Al Hilal… klabu nyingi zinashindwa kutimiza ndoto zake lakini hiyo haimaanishi sisi ni wabovu,” Ofisa Habari wa Yanga Sc, Ally Kamwe ndani ya SportsArena ya WasafiFm.



No comments:
Post a Comment