HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 22, 2022

'DARDY' YA UBABE NA HESHIMA, SIMBA NA YANGA



Na Swaleh Mawele


Wamba hawa hapa, moja ya dabi kubwa barani Afrika, mechi ya kuweka heshima kwa mpinzani, mara ya mwisho kwa miamba hii kukutana Yanga aliondoka na ushindi wa mabao 2-1 na kushinda taji la Ngao ya Hisani, Simba inaingia ikiwa na mabadiliko katika benchi lake la ufundi wakati Yanga ikiingia na sura zilezile.

Juma Mgunda anafanya vizuri na kikosi cha Simba tangu alipokipokea kutoka kwa Zoran Maki, amekuwa akibadilika kutokana na mazingira ya mchezo ( offensive and defensive ), mara nyingi katika kuzuia mfumo unakuwa 4-4-2 na wanaposhambulia wanabadilika na kutengeneza umbo la 4-2-3-1.

Nabi katika mechi nyingi za msimu uliopita alizocheza na wapinzani wake wa karibu ( Simba na Yanga ) amekuwa akitumia mfumo wa 'back three'( 3-5-2 ), katika mechi ya mwisho dhidi ya Simba alitumia back four ( 4-2-3-1 ), inawezekana akatu surpise katika mechi ijayo? ni kitu cha kusubiri na kuona.

Kiburi cha Mgunda kinaanzia kwenye eneo lake la kiungo, achana na pasi na utulivu wa Chama, achana na umahiri wa Inonga katika kuzuia kama mtu wa mwisho, utazame ubora mkubwa wa sasa wa Kanoute na Mzamiru katika eneo lao la kiungo wakati wakiwa na mpira au wanaposhambuliwa.

Bila ya mpira Okrah na Kibu wanashuka katika mstari wa pili wa kuzuia, timu inatengeneza umbo la 4-4-2, Israh na Zimbwe wanacheza karibu karibu na Okrah na Kibu, hapa Simba wamefanikiwa kuzifunga flanks zote mbili, Mzamiru na Kanoute wanalifunga eneo la kati.

Unajua utamu wa mechi utakuwa wapi? wakati ambao quality ya viungo wa Yanga itakaposhindana na ile ya Simba kwenye offensive patterns ( kushambulia ), nani atakuwa na ufanisi kulishinda kwanza eneo la katikati, ndipo muhimili mkuu ulipo kwa hizi timu zote mbili, ukilishika eneo la kiungo unajiweka karibu na kushinda mechi.

No comments:

Post a Comment

Pages