HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 19, 2022

SERENGETI GIRLS YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA




Na John Richard Marwa

Timu ya Taifa ya Soka la Wanawake Tanzania chini ya miaka 17 'Serengeti Girls ' imeandika historia mpya katika soka la kimataifa baada ya kutinga Robo Fainali ya Kombe la Dunia zinazoendelea nchini India.

Ikiwa ni kwa mara ya kwanza Tanzania kushiriki katika fainali za Kombe la Dunia Serengeti Girls wametinga hatua hiyo baada ya kufanikiwa kuvuna point nne za hatua ya makundi na kushika nafasi ya pili kwenye kundi lao ambalo kinara ni Japan mwenye point 9.

Mchezo wa leo Serengeti Girls waliwakabili Canada ambao walihitaki ushindj ili kusonga mbele huku Serengeti Girls wakihitaji alama moja.

Canada walikuwa kwanza kujipatia bao la Uongozi dakika ya 20 ya mchezo kabla ya Serengeti Girls kuchomoa bao hilo kabla ya dakika 45 za kwanza kutamatika.

Kipindi cha pili Serengeti Girls waliuchukua mchezo kiasi cha kiwafanya Canada kukosa ufanisi wa kuifungua safu ya ulinzi ya Serengeti Girls.

Matokeo mengine ambayo yameifanya Serengeti Girls kutinga hatua hiyo ni Ufaransa kushindwa kufurukuta kwa wababe Japan ambao wamefuzu hatua hiyo kwa ushindi wa asilimia miamoja.

Hii ni historia kwa Taifa la Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA kuweza kupeleka timu kwa mara ya kwanza na kutinga hatua ya Robo Fainali.

Serengeti Girls wanaungana na Timu ya Taifa Soka la Watu wenye Ulemavu Tembo Worries ambao mwaka huu walishiriki Fainali za Kombe la Dunia nchini Uturuki na kufanikiwa kutinga Robo Fainali huku ikishika nafasi ya saba kwa ubora wa viwango vya mchezo huo.

Kila la heri Serengeti Girls katika hatua inayofuata hakika Jamhuri ya Wapambananji iko nanyi katika kila hatua.



No comments:

Post a Comment

Pages