HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 21, 2022

TAÑZANIA YAUNGANA NA MATAIFA MENGINE KUPAMBANA NA UJINGA

 

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Juma Kipanga, akitoa hotuba yake wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la Elimu ya Watu Wazima 2022 yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Francis Michael, akiangalia kazi za vijana wanaosomea ufundi.

Karibu katika banda letu.

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Juma Kipanga, akifurahia wakati akipokea asali mbichi.





  Na Mwandishi Wetu


SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia imethibitisha kuungana na mataifa mengine Duniani kupambana na Ujinga.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Juma Kipanga wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la Elimu ya Watu Wazima 2022 amesema kwa kuzingatia kauli mbiu ya Elimu haina mwisho Tañzania inaungana na Dunia nzima kuutokomeza ujinga.


"Kwa kuzingatia kauli mbiu ya maadhimisho haya Tañzania inaungana na Dunia nzima katika kutafakari umuhimu wa kujua kusoma na kuandika na kuhesabu ili kujenga taifa safi lenye ubora wa mazingatio ya usawa na ujumuishi wa makundi yote katika utoaji wa Elimu" amesema na kuongeza

"Mipango na mfumo wa Elimu ya watu wazima  nayo imebadilika, kwa sasa mipango na mifumo ya Elimu ya watu wazima inajikita zaidi katika kutatua changamoto za wakati huu kama vile kukosa fursa ya Elimu ya Sayansi, Tekinolojia na ubunifu. Fursa za kupata ajira, Elimu ya ujasiriamali, utunzaji sa mazingira, haki za kijinsia watoto na wanawake"

"Serikali na wadau wengine nchini wameendelea kutumia Elimu ya watu wazima katika nyanja mbalimbali ili kuweza kulisaidia jamii kukabiliana na changamoto zilizopo." amesema.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia ambaye aliwakilishwa na Kamishna wa Elimu Dk. Lyabwene Mtahabwa amesema idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika imefikia asilimia 22, Ili kukabiliana na changamoto hii Wizara inaendela kutekeleza mkakati wa kikatiba wa kisomo na Elimu kwa umma uliozinduliwa rasmi  September 25, 2020"

"Mkakati huu unalenga kuboresha mikakati ya masomo kwa njia mbadala, Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia kupitia taasisi ya Elimu ya Watu wazima imendelea miradi mbalimbali.

"Miradi hii inatekelezwa kwenye mikoa nane amabyo ni Kigoma, Dodoma, Iringa, Tabora Mbeya, Njombe, Songwe na Dar es Salaam. Aidha katika awamu wa pili itatekelezwa katika mikoa sita ya Tañzania Bara, Simiyu, Shinyanga, Manyara, Pwani, Singida na Pwani." amesema.

No comments:

Post a Comment

Pages