HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 22, 2022

NI AMA ZAO AMA ZETU SERENGETI GIRLS DHIDI YA COLOMBIA



 

Na John Richard Marwa

Timu ya Taifa ya wasichana chini ya miaka 17,'Serengeti Girls U 17) Leo ni ama zao ama zetu dhidi ya Colombia mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Dunia huko nchini India.

Serengeti Girls watashuka mchana wa leo kusaka tiketi ya nusu Fainali dhidi ya Colombia mchezo unaotarajiwa kuwa mgumu na wenye mvuto mkubwa kwenye michuano hiyo.

Mtanange huo utalindima mchana wa leo majira ya saa 14:00 mchana kwa saa za Afrika Mashariki, Girls wanahitaji kupata matokeo ili kuandika to rekodi mpya kwenye Fainali hizo ikiwa ni mara ya kwanza kushiriki mashindano hayo.

Akizungumza  kuelekea mchezo huo wa Robo Fainal Kocha Bakari Shime 'Mchawi Mweusi' amesema matarajio ni kufanya vizuri katika hatua hiyo.

"Maandalizi ya kuelekea mchezo huu yamekamilika kwa asilimia kubwa, vijana wako tayari na sisi kama benchi la ufundi tumeshanaliza maandalizi ya kimbinu na masuala yote ya ufundi kulinganan na mpiznani Wetu.

"Tunafahamu tumepitia nyakati ngumu sana kufika hatua hii, hali ambayo inatuongezea nguvu za kiwakabili wapinzani Wetu. Bahati nzuri mpinzani wetu na yeye ni mara yake ya kwanza kucheza hatua hii hivyo tunayonafasi kuonyesha kitu." Amesema Shime na kuongeza kuwa.

"Watanzania wafahamu tuna matarajio makubwa  ya kufanya vizuri, tuko hapa kuipambania Tanzania na tutalifanya kwa vitendo siku ya leo. Kikubwa Dua na Sala zao waendelee kutuombea na sisi tufanye kazi yetu tutafanikiwa. " Shime

 

No comments:

Post a Comment

Pages