HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 16, 2022

YANGA KUMBUKENI MLA CHA UCHUNGU NA TAMU HAKOSI

 

Na John Richard Marwa


Wananchiiiiiiiiiiiiiii, waswahili wanasema, ' Mla cha uchungu na tamu hakosi' si mna uchungu nyie, si mnaumia nyie, si mnataka tamu nyie, basi badilisheni chungu yenu kuwa tamu.


Juzi si mmeazimisha miaka 23 ya Baba wa Taifa, tangu atutoke, basi leo azimisheni miaka 24 bila kucheza makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, naamini hata Nyerere atafurahi huko aliko.


Si mlilia kwa uchungu pale Lupaso kwa kutoka sare na hao Wamanga?! si mlitaka kuwapiga kama ngoma, mkajikuta mnawapigia CD na wao wakacheza sebuleni kwenu?!


Basi leo mko chumbani kwao, tena wanapotunzia silaha zao za kivita, za kwenu zikishindikana tumieni zao kuwaadhibu.  Nabi si anaongea lugha yao, basi simamisheni Jeshi la Wananchi hapo Khartoum.


Muonyesheni rafiki yenu Ibenge kuwa Wananchi wa Jamhuri ya Wapambananji hawajawahi shindwa vita, pigananeni hii ndio vita yenu ya mwisho.


Kumbukeni mnapambana na Al Hilal waliobora zaidi yenu,  lakini Jeshi lenu sio dhaifu kama wao. Pateni hasira za rafiki zenu Vipers wa Uganda si mlicheza nao wakawakaribisha Afrika msimu huu, basi wao safari imekolea wamempiga Katumbi na Genge lake pale Lubumbashi.


Profesa Nabi hili jina kwangu halijwahi kuwa na mashiko, mbona unakaa sana bongo, mbona unawatesa sana wabongo, nikuambie tu Sven, Gomes, Aussems walipita hapa wakaandika historia wakaondoka zao, basi anza kuandika yako leo Afrika iliandike upya jina lako.


Nyie wachezaji niwaambie tu kuwa 'Mshoni hachagui nguo' mbona mnachagua nguo za kushona wakati sikuku ni ya Wananchi, Wananchi hawachaguagi nguo ya kuvaa, wao wanachotaka  wapendeze na hizo kanzu za ugenini, mwageni jasho, vujeni damu zenu, Wananchi watatoka kuja kuwalaki paleee kwa Nyerere Ndege wanapotua.


Kila la heri Wananchi wa Jamhuri ya Wapambanaji.

No comments:

Post a Comment

Pages