HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 31, 2023

Vijana, wanawake Afrika ya kati watakiwa kujihusisha na ujasiliamali

Na Janeth Jovin


KIKOSI cha sita cha Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania (TANBAT 6), kimewataka vijana, wanawake na wanaume kujihusisha na ujasiliamali ili kuweza kujikwamua kiuchumi.



Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Ofisa habari wa kikosi hicho, Kapteni Mwijage Inyoma alisema kikosi hicho kimetoa kauli hiyo wakati wa mafunzo yaliyotolewa na kikosi hicho chini ya Wadau Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa (MINUSCA) kwa makundi hayo.


Alisema mamlaka ya Afrika ya Kati katika Wilaya ya Mambere kadei Berberati iliandaa mafunzo hayo na kwa viongozi wa mashirika ya kiraia kuhusu utambuzi na utekelezaji wa shughuli ya kuzalisha mapato.


"Kupitia mafunzo hayo, vijana, wanawake na wanaume wamepatiwa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa ujasiliamali katika kujiingizia kipato na kuacha kuwa tegemezi," alisema Kapteni Inyoma katika taarifa yake.

 Aidha alisema mafunzo haya yalifanyika kwa lengo la kuwaunga mkono kamati ya amani na Upatanisho ya mitaa mbalimbali katika nchi hiyo hasa wilaya ya Mambere Kadei.


"Washiriki hasa maundi haya tuliyoyajata wachangamkie fursa hasa kwa lengo la kubadilisha dira ya vikundi mbalimbali vya uzalishaji mali katika jimbo la Mambere Kadei," alisema


Hata hivyo alisema wadau kutoka Ofisi ya MINUSCA walitoa elimu kwa  washiriki na kuwaelezea faida ya dhana ya kuwa na vikundi vya ujasiliamali huku wakiwataka  kufanya utafiti wa soko wa bidhaa mbalimbali watakazo zitengeneza.



No comments:

Post a Comment

Pages