HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 04, 2023

CHAMA KIKUU CHA USHIRIKI KAGERA KCU 1990 LTD CHATOA NYONGEZA KWA WAKULIMA WA KAHAWA

Na Lydia Lugakila, Bukoba


Katika kuhakikisha wakulima wa Kahawa aina ya Robusta na Arabika Mkoani Kagera wanapata unafuu katika zao hilo Chama kikuu cha ushirika KCU(1990) LTD kimetoa nyongeza ya bei ya Kahawa hai(Organic) kwa kilo 1kwa shilingi 400 kwa Arabika na shilingi 300 kwa Robusta.




Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa chama kikuu cha Ushirika Kagera KCU 1990 Ltd Respicius John wakati akizungumzia mafanikio ya msimu wa kahawa 2022/2023 kwa kahawa hai organic katika Ofisi za chama hicho zilizopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.


Aidha Respicius ameongeza kuwa kwa msimu wa 2022/2023 bei ya Kahawa hai (ORGANIC) kwa kilo moja imefikia shilingi 5,300 kwa kilo 1 kwa Arabika na shilingi 4,700 kwa Robusta.


Hata hivyo katika nyongeza ya bei hiyo jumla ya  shilingi milioni 7,15 zimetolewa  kwa wakulima wa kahawa hai (organic).

No comments:

Post a Comment

Pages