HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 06, 2023

HALMASHAURI TATU ZANUFAIKA NA MSAADA WA VIFAA VYA SH42.3MIL KUTOKA BENKI YA NMB

 

 

Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Sebastian Waryuba (wa pili kushoto), akipokea vifaa tiba mbalimbali kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi (wa tatu kulia) katilka hafla ya makabidhiano ya vitanda nane vy kujifungukia na mashuka 60 kwa Hopsitali hya Wilaya ya Malinyi. Benki ya NMB imetoa msaada wa jumla ya thamani hya shilingi 42.3 milioni kwa halmashauri tatu za Morogoro, Mlimba na Malinyi zote za Mkoa wa Morogoro. Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Malinyi, Pius Mwelase na kulia ni Meneja wa Mahusiano ya Benki ya NMB na Serikali kwa Kanda ya Kati, Peter Masawe na wapili kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Malinyi, Omari Hamisi.  (NA MPIGA PICHA WETU).

Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Sebastian Waryuba (kushoto) na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi wakifurahia jambo na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwembeni baada ya benki hiyo kutoa msaada wa meza, viti, madawati na vifaa vya afya vyenye thamani ya sh42.3 milioni baada ya benki hiyo kutoa msaada wa meza, viti, madawati na vifaa vya afya vyenye thamani ya sh42.3milioni kwa Manispaa ya Morogoro, Malinyi na Mlimba mkoani hapa.


Na Mwandishi Wetu

 

Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali katika sekta ya afya na elimu katika halmashauri tatu za Mlimba, Malinyi na Manispaa ya Morogoro ikiwa sehemu ya benki hiyo kurejesha faida kwa jamii baada ya mwaka 2022 kupata faida ya kiasi cha sh429 bilioni huku ikitenga kiasi cha sh6.2bilioni kwa ajili ya kuhudumia jamii katika miradi ya maendeleo kwa mwaka huu hapa nchini.

Akizungumza katika shule ya sekondari Chita halmashauri ya wilaya ya Mlimba, Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kati, Nsolo Mlozi alisema benki hiyo kila mwaka imekuwa ikitenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kurejesha faida kwa jamii katika kutoa misaada sekta za afya, elimu na majanga ya asili yanayojitokeza na mwaka huu imetenga kiasi cha sh6.2bilioni.

Nsolo alisema kwa mwezi Machi mkoa wa Morogoro imenufaika na misaada katika sekta ya elimu na afya kwa kupata vifaa katika sekta hizo vikiwa na thamani ya sh42.3milioni katika halmashauri tatu za Manispaa ya Morogoro, Malinyi na Mlimba.

“Leo (Jana) NMB kwa mwezi Machi tumetoa vifaa katika sekta ya elimu na afya kama sehemu yetu ya kuunga mkono serikali miradi ya maendeleo baada ya sisi kupata faida na mwaka ulioisha tumeweza kupata faida ya sh429 bilioni na mwaka huu benki imeongeza fedha kwenda kwa jamii kutoka kiasi cha sh4bilioni hadi kufikia kiasi cha sh6.2bilioni hii ni kwa ajili ya kuhudumia jamii katika miradi ya maendeleo hapa nchini tukiwa na utamaduni wetu wa kurejesha faida kwa jamii.”alisema Nsolo.

Meneja Mahusiano Huduma kwa Serikali Benki ya NMB, Peter Massawe ametaja vifaa hivyo kuwa ni chuo cha Bigwa viti 100 na meza 100, shule ya msingi Sinyaulima Ngerengere vifaa vya ujenzi, Chita sekondari viti 50 na meza 50, Ngoheranga vita 50 na meza 50, shule ya msingi Mwembeni Malinyi madawati 50 na Hospitali ya wilaya Malinyi ikipokea vitanda nane vya kujifungulia akinamama wajawazito.

“Vifaa tulivyokabidhi vina thamani ya sh42.3milioni katika halmashauri tatu za Manispaa ya Morogoro, Malinyi na Mlimba katika sekta ya elimu na afya lakini Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa ni miongoni mwa waliopata viti 100 na mezo 100 kwa ajili ya kupunguza changamoto kwa wanafunzi na shule za msingi na sekondari ambavyo wamepata viti, meza na madawati.”alisema Massawe.

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Malinyi, Sebastian Waryuba alisema benki hiyo imekuwa msaada kwa serikali katika kutoa msaada sekta ya afya, elimu kutokana na kuipunguzia mzigo katika kutoa vifaa katika sekta hizo na kuomba taasisi nyingine za kifedha kuiga mfano kwa NMB kurejesha faida wanazopata kwenda katika jamii.

Kaimu Kurugenzi halmashauri ya wilaya ya Mlimba, Wakili Kulaba Dotto alisema baada ya benki hiyo kutoa misaada hiyo kwa shule za sekondari ya Chita na msingi Kalengakeru bado kuna upungufu wa meza na viti kwa shule za sekondari 1690.

“Viti 50 na meza 50 tulivyovipokea na madawati vitasaidia kupunguza upungufu kwa wanafunzi wetu kabiliana na na changamoto ya uhaba wa meza, viti na madawati katika shule zetu za msingi na sekondari na kwa sasa sekondari pekee kuna upungufu wa meza na viti 1690 kwa shule 31 ambazo zina wanafunzi 15,890 na meza na viti vilivyopo ni 14,200 hivyo tunaweza kuona kuna kila sababu ya kuhitaji msaada zaidi ili watoto wasome katika mazingira tulivu zaidi.”alisema Wakili Kulaba.

No comments:

Post a Comment

Pages