HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 27, 2023

UTT AMIS yadhamini mkutano wa Trampa na Tapsea

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi, Makatibu Mahsusi pamoja na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka kabla ya kufunga Mkutano wa Kitaaluma wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) pamoja na Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) uliofanyika Fumba Zanzibar Mei 27, 2023.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah (wa pili kulia) akimkabidhi tuzo Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Martha Mashiku, kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo wakati wa Mkutano wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) pamoja na Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) uliofanyika leo Mei 27, 2023 jijini Zanzibar. 

Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Martha Mashiku, akitoa mada kuhusu Akiba na Uwekezaji kupitia mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja inayoendeshwa na UTT AMIS wakati wa Mkutano wa Trampa na Tapsea uliofanyika jijini Zanzibar ambapo UTT AMIS ilidhamini Mkutano huo.









No comments:

Post a Comment

Pages