HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 26, 2023

KAMATI YA WAZIRI MKUU IMEKUTANA NA TAASISI ZA KIKODI NA UDHIBITI NCHINI

Kamati maalum ya kupitia changamoto za kibiashara nchini iliyoundwa na Waziri  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa imeendelea kukutana na Mamlaka zinazohusika Kodi na udhibiti nchini.


Kwa siku mbili za tarehe 23 na 25 Mei, 2023 kamati imekutana na Mamlaka ya Mapato (TRA) ,Mamlaka ya Bandari (TPA), Shirika la Viwango nchini (TBS) Pamoja na Tume ya Ushindani nchini (FCC).


Pamoja na mambo mengine tume ilitaka kupata kiini cha changamoto za kibiashara chini kama iilvyoibuliwa na wafanyabishara katika kikao chao na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. John Jingu amesema Kamati imeendelea na utekelezaji wa majukumu yake ambapo siku ya tarehe 23 kamati ilifika Bandarini eneo ambalo mizigo inapakuliwa na kuhifadhiwa na baadae Kamati imetembelea Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kukutana na Wadau mbalimbali wanaohusika  na forodha.


Dkt.  Jingu amesema Kamati imefanikiwa kuendela kukusanya maoni  na kufanya mahojiano na  Wataalam hao ambapo wametoa maoni mazuri yatakayosaidia kutatua changamoto zilizopelekea kuleta mgogoro na Wafanyabiashara.


Kamati pia imefanya mahojiano na wawakilishi wa makundi  ya Wafanyabiashara na Wadau mbalimbali ambao hawakuweza kupata nafasi ya kutoa maoni kwenye mkutano wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasimu Majaliwa na Wafanyabiashara  uliofanyika tarehe17 Mei , 2023 Jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini Bw, Hamis Livembe aliwataka taasisi na Mamlaka zinazofika mbele ya kamati kujikita katika kutafuta ufumbuzi zaidi badala ya kujitetea kwa kusimamia sheria za Mamlka husika.

‘’Ndugu zangu ,sisi siyo mahakama, nawaomba sote kwa Pamoja tujikite kwenye kutafuta suluhu ya changamoto zilizopo badala ya kila anayeitwa mbele ya kamati ama kujitetea au kutaja sheria za mamlaka au taasisi yake’’ alisisitiza Bw. Livembe.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo Bw. Martin Mbwana amesema kamati imeendelea kuleta matumaini na mafanikio makubwa ambapo wameweza kukubaliana na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kutoa baadhi mizigo ya Wafanyabiashara iliyokuwa imezuiliwa.

Mbwana amesema wafanyabiashara  wenye mizigo yao wafike ofisi za jumuiya ya Wafanyabiashara wakiwa na risiti na nyaraka mbalimbali za manunuzi zitakazo tumika katika utaratibu wa kukabidhiwa mizigo hiyo.

Pia amepongeza utaratibu unatumiwa kamati kushughulikia changamoto zao na hivyo wafanyabiashara wanapaswa kuendelea kuwa watulivu na kuendelea kuzingatia taratibu zilizopo ikiwa ni pamoja na kutoa risiti.


Kamati hiyo inaundwa na wajumbe 14 ambapo wajumbe saba ni wawakilishi wa makundi mbalimbali ya wafanyabiashara nchini na wajumbe wengine saba ni Kutoka Wizara na Taasisi mbali mbali zinazohusika na biashara nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages