Na Victor Masangu
Jumla ya
miradi 99 ya maendeleo ambayo imetembelewa na mingine kuzinduliwa na
kuwekewa mawe ya Asmsingi katika Mkoa wa Pwani imefanikiwa kupitishwa
yote bila ya dosari yoyote na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru
kitaifa.
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge wakati akimkabidhi rasmi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert
Chalamila katika eneo la tazara na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali
wa chama pamoja na serikali.
Kunenge
alibainisha kwamba mbio za Mwenge wa uhuru ukiwa katika mkoa wa Pwani
umeweza kukimbizwa umbari wa kilometa zipatazo 1201 katika Wilaya saba
na halmashauri zipatazo tisa.
Alifafanua
kuwa katika miradi hiyo mbali mbali ya maendeleo ambayo imeweza
imegusa katika sekta mbali imegharimu jumla ya kiasi cha shilingi
tilioni 4.4 ambazo zimetoka serikalini na nyingine kwa wadau wa
maendeleo.
Kunenge
alibainisha kuwa katika mbio hizo miradi tisa iliweza kufunguliwa na
mingine 15 kuzinduliwa huku miradi mingine 20 iliweza kupata fursa ya
kuwekewa mawe ya msingi huku miradi 15 imekaguliwa.
"Tunashukuru
tumemaliza salama kukimbiza mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wetu wa
Pwani na kwamba miradi yetu yote imeweza kupitishwa bila ya kuwa na
dosari yoyote Ile kutokana na kuwa na vigezo ambavyo vinatakiwa,"alisema
Kunenge.
Kwa Upande wake
kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Abdalah Kaim alisema kwamba
ameridhishwa na utekelezaji wa miradi mbali mbali ambayo wameweza
kuitembelea.
Alimpongeza
kwa dhati mkuu wa .Mkoa wa Pwani kwa kuweza kusimamia watendaji wake
katika suala zima la kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo itaweza
kuwasaidia wananchi.
Nao
baahi ya viongozi walioudhulia katika makabidhiano hayo hawakusita kutoa
pongezi kwa uongozi mzima wa Mkoa wa Pwani kwa kujitahidi kuibua miradi
hiyo ambayo imefanikiwa kupitishwa yote bila kukataliwa.
Walisema
kitendo cha miradi yote 99 kupitiwa na mbio za Mwenge na kufanikiwa
kupitishwa bila dosari yoyote ni mafaniko makubwa kwani inaonyesha namna
ya watendaji wanavyojitahidi kushirikiana bega kwa bega kwa maslahi ya
wananchi kwa ujumla.
Mbio
za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Pwani zimeweza kupita katika miradi
mbali mbali ya maendeleo ikiwemo kuweka mawe ya
msingi.kufunguliwa,kuzinduliwa na mingine kutembelewa katika sekta
tofauti.
No comments:
Post a Comment