HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 29, 2023

RC FATMA MWASSA ATANGAZA KIAMA KWA WATENDAJI WAZEMBE KAGERA

Na Lydia Lugakila, Bukoba

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatma Mwassa (pichani) amesema hatokuwa tayari kuwavumilia Watendaji Wazembe, wavivu,wacheleweshaji wa miradi ya Maendeleo, waongo wabadhilifu wa mali za umma.



RC Fatma ametoa kauli hiyo katika kikao na wakuu wa Taasisi za umma Mkoani Kagera kilichofanyika katika ukumbi wa Mkoa huo.

Fatma amesema kuwa hatokuwa tayari kuvumilia uzembe wa aina yoyote toka kwa watumishi watakaoonekana kukwamisha Maendeleo huku akiahidi kutotumia hata hata dakika moja kuwasamehe.

"Tutakukataa mara moja wewe mtumishi utakayeonesha uzembe katika kazi na tutaleta wanaotufaa hivyo ni lazima mkafanye au ufanye mabadiliko ya haraka kabla ya kukubaini" alisema Fatma.

Amesema anahitaji kuona Mkoa huo unatoka katika nafasi ya sasa kuichumi na kupanda juu huku akitegemea watumishi hao kufanya ubunifu wa haraka  katika miradi mikubwa ya Maendeleo.

aidha ameahidi kuhakikisha anaanza na miradi sugu iliyoonekana kukwama kwa muda mrefu ikiwemo ujenzi wa Stendi na Soko ambapo pia
amewakumbusha watumishi hao wajibu wao ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili maendeleo ya Mkoa huo yaonekane kwa haraka.

Hata hivyo jumla ya Taasisi 15 zimewasilisha tarifa za vitengo vyao na kubainisha changamoto katika utendaji wake ambapo Mkuu huyo wa Mkoa ameahidi kuanza kuzitatua mara moja.

No comments:

Post a Comment

Pages