Arusha.
Tarehe 20 Mei 2023: Kwenye mkutano wao mkuu wa 28 wa mwaka, wanahisa wa
Benki ya CRDB wameidhinisha mapendekezo ya Bodi ya Wakurugenzi ya
kulipa gawio la Shilingi 45 kwa kila hisa hivyo kufanya jumla ya gawio
kwa mwaka wa fedha 2022 kuwa Shilingi 117.5 bilioni.
Akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika katika katika Kituo cha Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC) huku wengine wakifuatilia ajenda zilizojadiliwa kwa njia ya mtandao, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt Ally Laay amesema gawio lililopitishwa ni sawa na ongezeko la 25% likilinganishwa na gawio la Shilingi 36 kwa hisa lililolipwa mwaka jana hali inayodhihirisha kuendelea kuimarika kwa pato kwa hisa ambalo mwaka 2022 limefika TZS 134.5.
Akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika katika katika Kituo cha Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC) huku wengine wakifuatilia ajenda zilizojadiliwa kwa njia ya mtandao, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt Ally Laay amesema gawio lililopitishwa ni sawa na ongezeko la 25% likilinganishwa na gawio la Shilingi 36 kwa hisa lililolipwa mwaka jana hali inayodhihirisha kuendelea kuimarika kwa pato kwa hisa ambalo mwaka 2022 limefika TZS 134.5.
“Kwa
mara nyingine tena, tunafurahi kupata matokeo mazuri kwa mwaka 2022
yaliyochangia kuongeza thamani kwa wanahisa wetu. Faida tuliyoipata
mwaka 2022 ni uthibitisho wa utekelezaji makini wa mpango mkakati wetu
wa miaka mitano wa 2018 – 2022. Benki ilipata faida ya baada ya kodi ya
Shilingi 351.4 bilioni sawa na ongezeko la 31% ikilinganishwa na
Shilingi 268.2 bilioni za mwaka 2021,” amesema Dkt Laay.
Vilevile,
Dkt. Laay amesema kampuni tanzu ya Burundi nayo inazidi kuimarika hivyo
kuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye faida ya kampuni mama. Kwa mwaka
2022, amesema Benki ya CRDB Burundi imepata faida kubwa zaidi tangu
lilipoanzishwa mwaka 2012. Kampuni hiyo tanzu ilipata faida ya Shilingi
23 bilioni mwaka 2022 ambayo ni sawa na ongezeko la 79.7% kutoka
Shilingi 12.8 bilioni iliyopatikana mwaka 2021. Kwa faida hiyo, kampuni
tanzu hiyo ilichangia 7.0% kwenye faida ya kampuni nzima.
“Nina
furaha kuwataarifu kwamba hivi karibuni tumepata leseni ya kuanza kutoa
huduma za fedha kutoka Benki Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(BCC). Vilevile, Benki yetu imeanzisha kampuni tanzu mbili mwaka huu
ambazo ni CRDB Bank Foundation na CRDB Insurance Company ikiwa ni benki
ya kwanza kuanzisha kampuni tanzu kamili a bima,” amesema Dk Laay.
Akizungumzia
utendaji wa Benki, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid
Nsekela amesema katika mwaka wa fedha 2022, waliendeleza juhudi za
kukuza mapato na wakafanikiwa kwa kiasi kizuri kwani mapato ya
uendeshaji yaliongezeka kwa 28% na kufika Shilingi 745.8 bilioni
yakichangiwa na kuongezeka kwa mikopo iliyotolewa. Kwa mwaka 2022,
uwiano wa mikopo chechefu ulishuka mpaka 2.8% hivyo kuwa ndani ya ukomo
uliowekwa kikanuni wa kutozidi 5%.
Mizania
ya Benki pia, amesema ilikua kwa 32% kutoka Shilingi 8.8 trilioni mwaka
2021 mpaka Shilingi 11.6 trilioni hivyo kuwa taasisiya kwanza ya fedha
nchini kuvuka Shilingi 10 trilioni. Ongezeko hilo, amesema limechangiwa
na kuimarika kwa amana za wateja zilizoongezeka kwa 26.4% na kufika TZS
8.2 trilioni kutoka TZS 6.5 trilioni za mwaka 2021.
“Juhudi
zetu za kuimarisha huduma zetu zilituletea mafanikio hasa katika kubana
matumizi kwani uwiano wa gharama na mapato uliimarika kutoka 66.7%
mwaka 2018 mpaka 49.4% mwaka 2022,” amesema Nsekela.
Nsekela
amesema ufanisi uliopatikana umewezesha kuwekeza zaidi kuimarisha
huduma kwa kuwekeza kwenye majukwaa ya kidijitali ambayo yanasaidia
kukidhi mahitaji ya wateja kwa kuwapa huduma wazitakazo mahali walipo na
kuzitumia kwa namna waitakayo. “Leo hii zaidi ya 95% ya miamala yote ya
benki inafanyika kidijiti hasa kupitia SimBanking, huduma za benki kwa
intaneti, na kwa zaidi ya mawakala 28,000 wa Benki ya CRDB,” ameongeza.
Katika
miaka mitano iliyopita, amesema Benki ilianzisha ubia wa kimkakati
ambao umechangia kwenye mafanikio yake kwa mwaka 2022. Katika kipindi
hicho, ubia huo umeiwezesha Benki ya CRDB pamoja na kampuni tanzu zake
kukuza mtaji, kuwa na teknolojia ya kisasa na kuboresha huduma hivyo
kukidhi matarajio ya wateja.
Kuhusu
mikakati ya baadae, Nsekela amesema Bodi ya Wakurugenzi imeidhinisha
mpango mkakati wa miaka mitano kuanzia mwaka 2023 – 2027 unaosisitiza
kujenga uchumi shirikishi, kuongeza thamani endelevu kwa wanahisa, na
kuingia katika ubia wa kimkakati ili kuikuza Benki na kuongeza ushawishi
wake sokoni.
Mpango
mkakati huo, amesema umetanguliza mbele maslahi ya wateja jambo
linalomaanisha Benki sasa inawekeza katika kuyatambua mahitaji ya wateja
na kuyafanyia kazi ili kukidhi matarajio yao.
Nsekela
amewashukuru wanahisa wa Benki hiyo kwa ushirikiano ambao wameendelea
kuipatia menejimenti na wafanyakazi wa benki hiyo, na kuwawathibitishia
kwamba Benki itaendelea kufanya vizuri ili kuwapa thamani ya uwekezaji
walioufanya na wanaoendelea kuufanya.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi, Dkt Ally Laay amesema mwaka 2022 walifanya
mabadiliko kadhaa ya menejimenti yanayoendana Sera mpya ya Rasilimali
Watu. Katika mabadiliko hayo, Bwana Boma Raballa aliyekuwa Mkurugenzi wa
Wateja Wadogo alipandishwa cheo na kuwa Afisa Mkuu wa Biashara
akichukua nafasi ya Dkt Joseph Ochieng Witts aliyestaafu.
Kutokana
na kupandishwa cheo kwa Bwana Raballa, amesema Bodi iliamteua Bwana
Bonaventure Paul kukaimu ukurugenzi wa wateja wadogo. Vilevile, Bwana
Godfrey Rutasingwa aliyekuwa anakaimu ukurugenzi wa Rasilimali Watu,
alithibitishwa katika nafasi hiyo.
Kwa
upande mwingine, wanahisa walipitisha kampuni ya Ernst & Young kuwa
mkaguzi wa nje wa hesabu za fedha kwa mwaka 2023. Vilevile, wanahisa
hao waliwachagua kwa mara nyingine tena Profesa Neema Morina Miranda
Naiman Mpogolo kuwa Wajumbe Huru wa Bodi ya Wakurugenzi.
Akizungumzia
gawio lililoidhinishwa, Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Benki ya CRDB
ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Vunjo, Dkt Charles Kimei amesema wanahisa
wamefurahia ongezeko la gawio lililopendekezwa. Dkt. Kimei aliongezea
kuwa kitendo cha Benki ya CRDB kutoa gawio kiila mwaka kimekuwa
kikiwavutia wawekezaji wengi ndani na nje ya nchi kuwekeza ndani katika
hisa za benki hiyo.
No comments:
Post a Comment