HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 03, 2023

MSANII EVANGELINE GODWIN A.K.A FABIYOLA AWAHIMIZA WASANII WENZAKE KUJISAJILI BASATA


BASATA-Dar es Salaam

Hayo yamezungumzwa na Msanii wa Ubunifu (Creative Artist)wa kutengeneza Sanaa mbalimbali  alipofika BASATA Kutoa shukrani zake Kwa Uongozi baada ya kupewa elimu juu ya faida zitokanazo na Baraza pale Msanii anapojisajili.

Tarehe 16 Machi 2023 Msanii Evangeline Godwin a.k.a Fabiyola alipata usajili BASATA wenye Namba:BST-9684-2023-1387 na hivyo kuwa rasmi katika kazi za Sanaa hapa nchini.

Aidha Fabiyola anasisitiza kuwa,alihamasika kujisajili BASATA kwa sababu alitaka kutambulika na kufanya kazi zake kialali.
Pili kupata fursa za kufanya kazi ndani na nje ya nchi lakini pia kuaminika zaidi katika Taasisi za Serikali.
Ameomgeza pia kwamba, kupitia BASATA atapata fursa ya kukutana na Wasanii mbalimbali katika kubadilishana mawazo.

Msanii Fabiyola alimkabidhi Zawadi ya Sanaa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Taasisi- BASATA Bi.Hannah Mwakalinga ambayo aliipokea Kwa niaba ya  Katibu Mtendaji wa BASATA .

 Bi.Hannah Mwakalinga Kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa BASATA amemkaribisha mdau  na kumhakikishia kwamba BASATA ipo tayari kumsaidia katika maeneo tofauti kama vile elimu juu ya kuendesha biashara kupitia mitandao ya kijamii, namna bora ya kuandaa miradi.


No comments:

Post a Comment

Pages