HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 04, 2023

WANANCHI KIUME SANA CAF CC

 NA JOHN MARWA


WAWAKILSHI wa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati klabu ya Yanga imeukosa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF CC licha ya kushinda (0-1) ugenini dhidi ya USM Alger ya Algeria.



Ulikuwa mchezo wa kufa ama kupona kwa Yanga SC baada ya kupoteza mtanange wa mkondo wa pili wa Fainali ya CAF CC msimu huu wa 2022/23.


Mchezo wa kwanza ulipigwa Benjamin Mkapa Yanga walikubali kipigo cha mabao (1-2) ambao ndio umeamua mshindi kwa bao la ugenini. Ambalo Alger walipata mabao mawili na Yanga wamepata moja huku matokeo ya jumla yakiwa ni (2-2).


Yanga wanamaliza nafasi ya pili huku USM Alger wakitawazwa kuwa mabingwa wapya wa CAF CC.


Matokeo hayo yamepokelewa kwa vilio na simanzi kwa Kocha Mkuu Nasreddine Nabi pamoja na mshambuliaji Fiston Mayele baada ya kipyenga cha mwisho cha mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

Pages