HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 14, 2023

KMC FC KUTIMKIA ZANZIBAR IKIINGIA KAMBINI KESHO

Na Mwandishi Wetu

Kikosi cha Timu ya Manispaa ya Kinondoni KMC FC kesho kitaingia kambini tayari kuanza safari ya kuelekea visiwani Zanziba kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara 2023/2024 unaotarajiwa kuanza Agosti 15 mwaka huu.

Wakati kikosi cha kikirajiwa kuwasili kambini hapo kesho, siku ya Jumapili  ya Julai 16 wachezaji wote watafanyiwa vipimo vya  afya  sambamba na kutambulisha kikosi kipya cha msimu wa 2023/2024.

Vijana wa Kino Boys  wataondoka Julai 18 kwenda Zanzibar ambapo itaweka kambi huko kwa muda wa wiki mbili na baada ya hapo itarejea Jijini Dar es Salaam na kuanza safari ya kwenda mkoani Morogoro ambapo itakuwa huko kwa siku kadhaa na kisha kurejea tena kwa ajili ya kuendelea na maandalizi huku ikisubiria ratiba ya kuanza kwa maimu.

KMC FC ambayo kwa sasa itakuwa ikinolewa na kocha Mkuu Abdihamid Moallin ambaye alitangwa Jumatano ya Julai 12 mwaka huu, ikiwa huko visiwani Zanziba itakuwa na programu mbalimbali kulingana na mahitaji ya kocha kwa lengo la kukinoa kikosi hicho kuelekea katika msimu mpya unaokwenda kuanza hivi karibuni.

“Maandalizi ya kuanza kwa msimu mpya yamekamilika kwa asilimia kubwa, na kesho kikosi kitaingia kambini kuanza safari ya kwenda Zanziba , tukiwa huko tutafanya mambo mbalimbali kwa ajili ya kuwajenga wachezaji wetu kadiri ambavyo kocha Moallin ataona inafaa kwa sababu tunakwenda kwenye msimu wenye ushindani mkubwa zaidi tofauti na ule uliopita.

"Aidha kuhusu usajili KMC FC hadi sasa tumekamilisha jumla ya maingizo mapya ya wachezaji nane ambao ni Golikipa Wilbol Maseke, Rahimu Shomary, Fredy Tangalo, Vicent Abubakari, Andrew Sinchimba, Juma Shemvuni, Roges Gabriel pamoja na Twalib Mohamed.

"Kwa upande wa wachezaji ambao wamemaliza mikataba yao na hivyo hawatakuwa sehemu ya msimu unakuja ni pamoja na Nurdin Balora, David Kisu Mapigano, Mohamed Samata, Frank Zakaria ambaye alitoka Singida Big star kwa mkopo, Issac Kachwele, Kelvin Kijili, Steve Nzigamasabo, Ally Ramadhan pamoja na Matheo Antony.

“ Ukiangalia aina ya wachezaji ambao tumewasajili msimu huu ni watofauti kwa sababu hasa tumezingatia mambo mengi hususani uwezo na ubora lakini pia umri sio mchezaji ambae ameshapita kwenye vilabu vingi hapana, tunahitaji kuwa na wachezaji wenye kiu ya mafanikio kwa masilahi ya Timu yetu na Manispaa kwa ujumla." Amesema Christina Mwagala Ofisa Habari na Mawasiliano wa KMC FC.


No comments:

Post a Comment

Pages