HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 14, 2023

WATANZANIA WAWE MAKINI NA MAKUNDI HAYA

NA DENIS MLOWE, IRINGA

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Richard Kasesela amewataka Watanzania kuwa makini na makundi manne ambayo yamekuwa yakizungumzia kuhusu  suala la uwekezaji wa bandari ya jiji Dar Es Salaam.

Kasesela aliyaorodheha makundi hayo kuwa ni kundi la kwanza ni ambalo linajua umuhimu wa  bandari kuweza kufanya kazi kwa kupitia mwekezaj, kundi la pili ni la wadau wanaonufaika na ubovu wa bandari ambao kwa kiasi kikubwa ni wengi sana na kundi hili ndio linatikisa uchumi wa nchi kwani kundi hili unaweza unaweza kwenda bandarini bila hela ukarudi nyumbani na milioni 100 kwa kucheza na makaratasi..

Alisema kuwa endao mwekezaji DP world akija kundi hili la pili litakufa mara moja kwani kutokana na utendaji kazi wao hata pini iliyomo kwenye meli itajulikana hali ambayo itafanya kundi hili la pili kupoteza magendo yao hali ambayo wamekuwa wakileta ugumu kwenye uwekezaji.

Aliongeza kuwa kundi la tatu  la tatu ambalo limekuwa likizungumza vibaya ni la wanasiasa ambao wamekuwa kitafuta kiki za kisiasa kupitia DP WORLD na kuna wengine wameshapotea kwenye siasa sasa limeona hii bandari ndio njia ya kuruka kuelekea kwenye kurudi kisiasa tusiwasindikize bila kujua wanakwenda kufanya kwani hapa linatengenezwa wasaliti wa uchumi wan chi.

 Alilitaja kuwa kundi la nne kwenye sualala bandari ni la Bendera Fuata upepo ambalo jambo lolote likienda kushoto wao wapo likienda kulia pia wapo sasa hatari ya kundi hili la nne linaweza kuitwa kwenye maandamano wapo wasiandamane wapo hawa ndio changamoto kubwa kwenye uwekezaji.

Kasesela ambaye ni mkuu wa wilaya Mstaafu wa wilaya Iringa, akizungumzia kwa upande mwingine kuhusu suala la bandari alisema kwamba alikuwa mmoja ya wajumbe saba waliounda kamati ya kuchunguza ubadhilifu na udhaifu wa bandari ya Tanzania na taarifa ya kamati ilipendekeza kuwe na mwekezaji mwingine.

Alisema kuwa katika uendeshaji wa bandari hiyo walibaini kwamba gati namba 1 mpaka namba 7 kulikuwa na uovu mkubwa kiutendaji kwenye bandari hiyo hivyo kuona mwekezaji kama DP World amekuja watanzania wanatakiwa kuelewa manufaa makubwa kwa mwekezaji ambaye ni bora duniani.

Alisema kwamba watanzania wanatakiwa kuelewa kwamba wabunge waliweza kujadili jambo la manufaa kwa nchi na kuwaepuka wale ambao wamekuwa wakizungumza kwa misingi ya kupinga suala la bandari ili mradi kutafuta kiki na kutolea mfano mwanasheria Madeleka ambaye amekuwa akizungumza sana suala hilo kwa kuwapotosha watanzania.

Kasesela alisema kuwa Watanzania wamekuwa na hofu na ardhi, kwamba anayekuja atachukua ardhi jambo ambalo sio kweli  na hakuna mwekezaji aliyepewa ardhi kwa sababu hata kwenye sheria za uwekezaji, mwekezaji hapewi ardhi bali anapata kibali cha kukaa juu ya ardhi, na analipa kodi ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi.

“Watanzania waelewe kwamba hii Bandari sio ya watanzania pekee Tanzania tunaimiliki ila inasaidia nchi saba na endapo tukiacha nchi hizo ziondoke kutokana na bandari kutokuwa na ufanisi basi tusishangae ikawa bwawa la kuogelea kwani nchi nyingine majirani zitawekeza kwenye ufanisi bora” kwahiyo kuna biashara kubwa sana ambayo inaweza ikafanyika"

Alisema kuwa athari za kutokuwa na ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam ni pamoja na  meli kusubiri muda mrefu nangani ambako kunasababisha kuongezeka kwa gharama ya kutumia bandari ya Dar es Salaam, kwa mfano gharama za meli kusubiri nangani kwa siku moja ni takriban Dola za 25,000 kwa sik.

 

No comments:

Post a Comment

Pages