HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 14, 2023

NASSIBU RAMADHAN LORENI JAPHET WAPIMA UZITO KUZICHAPA KESHO PAMBANO LA PAYBACK NIGHT KINESI DSM

 Nassibu Ramadhan na Loren Japhet Wa pima Uzito Tayari Kuzichapa Kesho Kwenye Pambano La PayBack Night Litakalopigwa Julai 15,2023 Katika Uwanja Wa Mabibo Dar es salaam.

Wakizungumza Mara Baada Ya Kupima Uzito Mapema hii Leo Katika Viwanja Vya Mabibo Las Vegas Wamesema Wamejiandaa Vizuri Hivyo Watanzania Watarajie kuona Burudani Yenye Ladha Ya Aina Yake Kwenye Pambano Hilo.


Kwaupande wake Mratibu Mkuu Wa Mapambano Tanzania Meja Seleman Semunyu Amesema Maandalizi Maandalizi Makubwa Yamefanyika Hivyo Siku Ya Kesho Watanzania Watarajie kuona Mabondia Wakionesha Burudani Ya Aina Yake Yenye Ladha Ya Masumbwi Duniani.

Mapambano Kumi Makali Yatapigwa Huku Mabondia  Nassibu Ramadhani kuoneshana Umwamba Wa Ulingo Dhidi Ya  Loren Japhet, Ramadhani Iddi kuzichapa na Peter Toshi Wa Mbweni JKT, Hassan Ndonga na Tasha Mjuaji,James Kibanzange na Ramadhani Pido Katika Pambano PayBack Night Julai 15,2023 kwenye Uwanja Wa Kinesi Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages