HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 14, 2023

WANACHUO MALYA MABALOZI WA MICHEZO NCHINI–DKT CHANA

Adeladius Makwega-MWANZA

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini, mhe. Dkt Pindi Chana, Julai 14, 2023 ametembelea Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya na kukagua miradi kadhaa ya maendeelo inayoendelea kujengwa chuoni hapo, chini ya fedha za Serikali Kuu zinazotolewa kila bajeti ya kila mwaka na kusema kuwa anawapongeza sana wanachuo wa chuo hiki kwa kuchagua kusoma michezo na wao ni mabalozi wa michezo nchini.

 Akizungumza huku akishangiliwa na wanachuo hao Waziri Dkt. Chana alibainsiha kuwa,

“Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatamka wazi kuwa michezo inapaswa kuendelezwa , na kusomea michezo ni mojawapo ya maendeleo hayo. Ualimu wa michezo ni muhimu sana maana hata katika tiba unatumika pia. Juzi kuna mgonjwa amenipigia simu, akiomba namba ya mwalimu aliyesomea mazoezi ya viungo ili amsaidie maana alipewa maagizo daktari kufanya hivyo.”

Katika kikao hicho Waziri Dkt. Chana alipata nafasi ya kujibu maswali kadhaa yaliyoulizwa na wanachuo hao ambapo Ladislausi Lunguya Rais wa Serikali ya Wanachuo na Ndinagwe Sungura Makamu wa Rais wa Serikali ya hiyo ya Wanachuo waliomba kupatiwa vifaa vya michezo.

Waziri Dkt. Chana alijibu kuwa kwa hakika hoja hiyo ya vifaa tayari alielezwa na Mkuu wa Chuo Richard Mganga katika ripoti aliyomsomea asubuhi ya Julai 14, 2023 hilo litapatiwa ufumbuzi.

Kwa upande wao wanachuo Lucy Malisa na Eliasi Mashenzi ambao walifunga ukurasa huo wa maswali kwa pamoja wao walijikita katika kuomba kuondolewa kwa utaratibu wa kushushwa madaraja kwa walimu walisomea mIchezo pindi wanapohitimu na kurudi mkazini wakiwa mafisa michezo,huku wakiomba kuongezwa kwa wakufunzi maana mkufunzi mmoja anakuwa na mzigo mkubwa wa vipindi na pia wakishauri wale wanachuo wasio na ajira wanasoma chuoni hapo kupatiwa ajira.

“Tayari Wizara yangu na wizara zote zinazohusika na suala na wale walimu wanaopanda na kuwa maafisa michezo wasishushwe ngazi zao za mishahara linafanyiwa kazi. Tumeshafanya vikao kadhaa juu ya suala hilo .”

Awali wakati wa kumkaribisha Waziri Dkt. Chana, Mkuu wa Chuo hiki ndugu Richard Mganga alimshukuru Waziri Dkt. Chana kwa kufika hapo na kuzungumza na wanachuo hao 261, huku akitia shime kuwa michezo inalipa na wanachuo hao kadhaa sasa wameshaonja utamu na matunda ya michezo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Micezo nchini Ali Mayay Tembele alisema kuwa anampongeza Waziri Dkt. Pindi Chana kwa kujituma katika kuikamilisha adhima ya taifa ya maendeleo ya michezo nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages