HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 03, 2023

ROBERT MUNISI APITA KWA KISHINDO UCHAGUZI KIBAFA

Na Khadija Kalili, PWANI

ROBERT Munisi  kwa  mara ingine  tena ameibuka na ushindi wa nafasi ya Mwenyekiti  wa Chama Cha Soka Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani  katika uchaguzi  uliofanyika leo Julai 2  mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa KIBAFA, amesema amekuja kivingine ikiwa ni pamoja na kufanya mgawanyiko katika utendaji jambo ambalo imemlazimu kuunda Kamati  mbalimbali ambazo zitakuwa tendaji katika masuala ya takayohusu KIBAFA, Kamati  hizo ni  pamoja na kuundwa kwa Bodi ya Wadhamini itakayoongozwa na Mwenyekiti wake Rugemalira Rutatina, Makamu  Katibu ni  OCD  Mlandizi Julieth Lyimo Wajumbe ni Meja Jenerali  Bahati  na Mohammed Sumaye.
 Aidha Munisi amezitaja Kamati zingine  kuwa ni pamoja na Kamati ya  Nidhamu na Maadili , Kamati itakayosimamia Soka la Vijana, Kamati ya Soka  la Vijana na Wanawake,Kamati ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) pia amemtangaza  Hassan Mtengefu kushika nafasi ya Meneja Habari wa KIBAFA.

Aidha  nafasi ya Makamu  Mwenyekiti KIBAFA  imekwenda kwa David Mramba, Katibu Daudi Mhina na  Katibu Msaidizi ni  Omari  Abdul Pumzi Mweka Hazina ni  Laurent Didas
 Naye Katibu  Mkuu wa Chama Cha  Soka Mkoa wa Pwani Mohammed  Masenga ametoapongezi kwa KIBAFA kwa kufanya uchaguzi uliokuwa wa wazi na haki huku akitoa rai kwa wanachama kushirikiana  vyema na uongozi ulioingia  madarakani  ipasavyo  huku akisisitiza kuwa wawe na moyo wa kujitolea zaidi kwa sababu  kazi ya mpira ni ya kujitolea zaidi na kuhakikisa soka Wilayani  kibaha linakua  na kuamsha hamasa zaidi kwa vijana.

MWENYEKITI wa KIBAFA, Robert Munisi (wa pili kushoto), akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa kuwa  Mwenyekiti  wa Chama Cha Soka Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani.

No comments:

Post a Comment

Pages