HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 04, 2023

WA SENEGAL WATUA AZAM KUONGEZA NGUVU

 

Na John Richard Marwa


Klabu ya Azam imemtambulisha makocha wawili raia wa Senegal ikiwa ni kuendelea kulijenga benchi la ufundi la Kocha Mkuu Youssouph Dabo.


Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Azam FC imebainisha kuwa makocha hao, mmoja ni Kocha wa Makipa na mwingine ni mtathimini wa viwango vya wachezaji.


"Tunayo furaha kuwatangaza wataalamu wawili wapya kwenye benchi letu la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Youssouph Dabo.  

Tunamtambulisha, Khalifa Ababakar Fall (wa pili kutoka kulia), kuwa Kocha mpya wa Makipa na Ibrahim Diop, kama Mchambuzi wa mechi (Video Analyst), wote raia wa Senegal.


"Wataalamu wote wawili wamesaini mkataba wa miaka mitatu kila mmoja." Imeeleza taarifa hiyo.


Makocha hao wameungana na kikosi tayari kwa maandalizi ya kuelekea msimu ujao wa 2023/24 ambao Azam FC itakuwa na kibarua kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF CC.

No comments:

Post a Comment

Pages