HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 23, 2023

TABORA UNITED KAZI IMEKAMILIKA KUIVAA SINGIDA BIG STARS

Na John Marwa 


UONGOZI wa klabu ya Tabora United (Kitayosce FC) umesema tayari wameshughurikia sakata la  wachezaji wao wa kimataifa kukosa vibali na sasa watakuwepo kwenye mchezo wa  pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Fountain Gate FC hapo kesho.


Katika mechi ya kwanza ya Ligi hiyo, Tabora United walishindwa kutumia wachezaji wao wakigeni akiwemo Papy Tshishimbi aliyewahi kucheza Yanga, nyota wengine ni Andy Bikoko (SM Sanga Balende -DR Congo),  Toauya Jean kutoka klabu ya Rajaa ya Burundi na Lumiere Banza kutoka TP Mazembe.


Meneja wa timu hiyo, Rashid Hassan alisema baada ya kutokea sintofahamu kwa kukosa wachezaji wakigeni katika mchezo na Azam FC kwa sababu majina yao hayakuwepo kwenye mfumo, tayari wameshafanyia kazi na mechi dhidi ya Singida Fountain Gate FC watakuwepo.


Amesema kulikuwa na chanagmoto ya kiuongozi na wameshaifanyia kazi na tayari wachezaji na timu imeweka kambi Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao dhidi ya Singida Fountain Gate utakaopigwa Agosti 31, mwaka huu.


“Kila kitu kimekwenda vizuri wachezaji wetu wapya tuliowasajili tumeshawaingiza kwenye mfumo na tunajipanga kwa mechi ijayo ya ligi kuhakikisha tunafanya vizuri na kupata matokeo mazuri baada ya kupoteza mechi ya kwanza na Azam FC,” amesema Meneja huyo.


Naye Kocha Mkuu wa kikosi cha timu hiyo, Goran Kopunovic amesema kabla ya kwenda kuweka kambi Morogoro alifanya kikao na viongozi wake na kumuhakikishia hakutakuwa na changamoto yoyote ya kukosa wachezaji katika mechi ijayo.


Akizungumzia susla lake la kimkataba na kumuahidi kufanyia kazi kwa kuweza kukamilisha kile ambacho walikubaliana katika mkataba wao walioingia.


“Nimezungumza na viongozi wangu kuhusu makubaliano yetu lakini pia mustakabali wa timu kwa wachezaji ambao tume wasajili kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri niweze kuwatumia kwenye mechi yetu ijayo dhidi ya Singida Fountain Gate FC, limefanyiwa kazi na sasa ttuko Morogoro kwa ajili ya maandalizi, “ amesema Kocha Goran.

No comments:

Post a Comment

Pages