HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 30, 2025

CCM: Tunajenga masoko, tunawapa mikopo isiyo na riba

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), inatoa kipaumbele cha mikopo kwa wafanyabiashara wadogo waliopo katika masoko mapya yaliyojengwa katika halmashauri za miji yote ya Unguja na Pemba, Zanzibar.


Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema lengo la kujengwa masoko ni kuwapatia sehemu bora ya kufanyiabiashara na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliona pia ni lazima wapatiwe mikopo isiyo na riba.

Dkt. Mwinyi ambaye pia ni mgombea Urais katika uchaguzi mkuu ujao 29 Oktoba 2025 kupitia CCM, pia anataka wapewe nafuu ya kodi katika hayo masoko kwani yamejengwa na pesa za serika
Ii hivyo hakuna haraka ya kutaka masoko yazalishe faida haraka kupitia kodi za wajasiriamali hao.

Mwenezi Mbeto anabainisha kuwa riba ya mikopo hiyo inalipwa na serikali na kuna aina mbili za mikopo ambao ni ile inayotolewa na Wakala Uwezeshaji Kiuchumi Zanzibar (ZEA) na ya Halmshauri za Miji.

" Tuna mikopo tunaiita 4,4,2 ikiwa na maana vijana asilimia 4, kinamama pia hizo 4 na mbili ni kwa ajili ya wenye ulemavu kiwango ambacho ni kikubwa kuliko halmashauri zingine popote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" alisema.

Mbeto alisema zaidi ya Tsh.Bilion 55 zimetumika kujenga masoko hayo katika halmashauri na TSh.Bilioni 16 kwa masoko ya kimkakati ambayo ni Mwanakwerekwe, Chuini, Jumbi na hivi karibuni litazinduliwa la Mombasa, ambalo linajengwa na Mfuko wa Taifa wa Pensheni za Wafanyakazi Zanzibar (ZSSF).

"Yote hayo yamefanywa kuwawezesha wananchi kupata fursa ya kujitengenezea kipato lakini hilo wenzetu (upinzani) hawalioni" alisema.


 



 

No comments:

Post a Comment

Pages