NA DENIS MLOWE, IRINGA
MGOMBEA
ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya CCM, Fadhili Ngajilo
ameahidi wananchi wa kata ya Nduli kuwa akichaguliwa kuwa mbunge
atahakikisha kuwa eneo la Mapanda kutajengwa viwanda vidogo vidogo ili
kuzalisha ajira kwa vijana.
Akizungumza katika
mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM wakiwemo
Mratibu wa Kampeni wa Jimbo hilo, Salvatory Ngerela, na aliyekuwa meya
wa manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada, Mgombea ubunge Fadhil Ngajilo
alisema kuwa lengo kuanzishwa viwanda hivyo ni kuzalisha bidhaa na
kuchochea ajira kwa jamii hususani vijana na kuongeza mzunguko wa fedha
katika kata ya Nduli.
Ngajilo alisema kuwa
kufanikisha hayo katika kata ya Nduli wakumbuke kuwa maendeleo hayaji
bila ushirikiano wa karibu kati ya viongozi na wananchi na kuwataka
kumpa ushirikiano kuwaletea maendeleo yao.
Akizungumzia
kuhusu changamoto ambazo haziitaji kupelekwa hata bungeni kama maji na
umeme alisema kuwa kila kitu kipo sawa kinachohitajika ni watu
kupelekewa umeme na maji kwani miundo mbinu ipo tayari.
"Nduli
tutashughulika na kila changamoto zote ambazo mgombea udiwani
ameniagiza hivyo kura zenu ndio ukombozi wenU suala la maji,umeme ni
jambo ambalo tunalimudu kwani changamoto kubwa ni umeme kuwafikia watu
kwani miundo mbinu ipo" Alisema
Aliongeza kuwa
kazi yangu ni kuhakikisha mnapata maendeleo na Nduli changamoto ya
mawasiliano ya simu ni ngumu sana hivyo hilo tutashughulika nalo hapa
hapa sio kutupeleka bungeni kwani nikiwa mbunge mambo makubwa ndio
anatakiwa kupelekewa rais kama kuongezea nguvu kwenye ujenzi wa
barabara.
Alisema kuwa kata ya Nduli mnahitaji
barabara nzuri iwe za rami hadi Changalawe hivyo endapo akichaguliwa
kuwa mbunge atahakikisha zinajengwa ili ziweze kupitika nyakati zote.
Aidha
aliongeza kuwa endapo atachaguliwa kuwa Mbunge atahakikisha wakazi wa
kata ya Nduli atashughulikia changamoto ya wakulima kuhusu mbolea
kuwafikia kwa wakati na yenye ubora.
Aidha atahakikisha Kata ya Nduli linajengwavl Soko ambalo litawasaidia wakazi wa kata hiyo.
Ngajilo
alibainisha kuwa endapo atakuwa Mbunge atapigania mkoa wa Iringa kuwa
jiji hivyo ni vita kubwa ambayo inahitaji kuwa kamili katika Miundo
mbinu na kuendelea kutatua changamoto zilizopo.
Vilevile
alisema kuwa Nduli ni kata ya kimkakati kuwepo kwa kiwanja cha ndege ni
faida kubwa atahakikisha kuwa uwanja unabadilishe maisha watu wa Nduli
hivyo tutakuwa na vikao ili kuona tunabadilisha vipi maisha kupitia
uwanja wa ndege.
Aidha alisema kuwa atahakikisha wananchi wa
Kata hiyo wanarasimisha ardhi kuweza kufanya kazi zenu kwa amani na
nyumba zenu ziwe rasmi hivyo tutafanyia kazi kwa kushirikiana na diwani
Ngajilo
aliwataka wananchi wa Iringa Mjini kujitokeza kwa wingi kupiga kura
kwa Rais, wabunge na madiwani wa CCM, akisema kura nyingi ndizo
zitakazoongeza hamasa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kwa
upande wake mgombea udiwani wa Kata ya Nduli, Bashir Mtove alisema kuwa
ataendelea kuboresha barabara za vumbi ili ziweze kupitika muda wote.







No comments:
Post a Comment