Na Mwandishi Wetu, Pemba
Kampuni sita zimepewa zabuni za ujenzi wa barabara zaidi ya kilometa 1,300 Unguja na Pemba ndani ya miaka mitano ya Dkt. Hussein Ali Mwinyi tofauti na madai ya viongozi wa ACT Wazalendo katika kampeni zao majukwaani kuwa tenda zote imepewa Kampuni moja, jambo ambalo si kweli.
Akizungumza katika kipindi cha Ukweli wa Mambo kinachorushwa na SK Online Televisheni, 21 Septemba 2025, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema, kuna Kampuni sita ambazo zinatekeleza na zingine zimemaliza miradi ya ujenzi wa barabara, Unguja na Pemba ikiwa ni sehemu iliyopitiliza ya utekeleza wa malengo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025/2030.
Mbeto alisema madai ya ACT Wazalendo waliyotoa wakiwa katika moja ya mikutano yao Pemba ni uzushi, upotoshaji kudanganya umma kwani Kampuni walioitaja na kudai ndio pekee si kweli kwani zabuni za wazi ziliitishwa na makampuni sita kati ya hayo mawili yakiwa ya kizalendo wamepewa kandarasi katika ujenzi wa miradi tofauti.
Kuhusiana na tuhuma hizo kama hizo za ACT hivi sasa kuhusiana na kutotangazwa kwa baadhi ya zabuni za miradi ziliwahi pia kutolewa ufafanuzi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati wa mkutano na wanahabari Ikuu Zanzibar, 2 Septemba 2025.
alibaisha kuwa kulingana na sheria za manunuzi na ugavi kuna aina tatu zabuni ambao ni za wazi, jadiliwa na teuliwa na kuna tenda ambazo hutangazwa na kampuni yoyote yenye kukidhi vigezo inaweza kuomba.
Kuna aina ya pili ya zabuni ambayo timu maalum hushindanisha kampuni mbili hadi tatu na kuchagua mojawapo na nyingine ni ya kuteua kampuni moja yenye uwezo na uzoefu na hilo hufanyika baada ya kikosi kazi kujiridhisha na utendaji wake ikiwa ni pamoja na kukagua miradi ambayo wamewahi kuitekeleza.
Mwenezi Mbeto akizungumzia madai hayo ya ACT, alisema kuwa msimamizi wa Ilani hiyo, Rais Dkt. Mwinyi alitaka miradi itekelezwa kwa kasi kubwa na imalizike kwa wakati tofauti na miaka ya nyuma ambako barabara moja ingejengwa kwa miaka mitano hivyo ilikuwa lazima ziitishwe zabuni na yachaguliwe makampuni yenye uwezo.
“Bila miundombinu mizuri ni vigumu kufanya maendeleo hivyo ndio maana Rais Dkt. Mwinyi, akaona awarahishie wananchi jinsi ya kufanya shughuli zao za kiuchumi” alisema na kuongeza kuwa ndio maana hata kandarasi zimetolewa kwa makampuni tofauti ya nje na ndani ya nchi na zabuni zilikuwa za wazi.
Alisema kuna kampuni za kizalendo ikiwemo kongwe ya Mwananchi Engineering Contruction Ltd (MECCO), ORCUR ya Uturuki, CCECC ya China na Propav Infrustructure ya Brazil ambayo inaenda kujenga Uwanja wa Ndege wa Kisasa, Pemba na barabara ya njia nne yenye urefu wa kilometa 43.4 kutoka Chake hadi mkoani, Pemba zimeshinda zabuni katika miradi ya barabara katika maeneo tofauti.
“Tena uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja huo na barabara hiyo ya njia nne, Rais Dkt. Mwinyi ataufanya 25 Septemba 2025” alisema na kuongeza kuwa hao wanaosema ni Kampuni moja pekee ni kuwadanganya, wananchi.
Alizitaja Kampuni zingine zinazotekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara Unguja na Pemba ni pamoja na IRIS inayojenga kilometa 279.95 Zanzibar nzima ikiwa imepewa kilometa 134 Pemba na Kampuni ya kizalendo ya Orva Z kilometa zaidi ya 10.5. Mgelema/Wambaa na itapita maeneo ya Gongoni, Msiwaki, Mwapula na vijiji vingine.
Mbeto alisema fedha za ujenzi wa miundombinu hiyo zinatokana na mapato ya ndani kupitia Mfuko wa Barabara (Road Fund) ambapo kuna kiasi cha pesa kinakatwa katika kila lita ya mafuta, ada za matumizi ya njia (Road Licence) na hata inapotokea kuazimwa kwingineko urejeshaji ni rahisi kutokana na vyanzo hivyo vya mapato kubakia katika ujenzi wa miundombinu pekee.
September 22, 2025
Home
Unlabelled
CCM yakanusha Kampuni moja kupewa kandarasi zote Zanzibar
CCM yakanusha Kampuni moja kupewa kandarasi zote Zanzibar
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.


No comments:
Post a Comment