Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Mgombea wa Kiti cha Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuwajengea soko la kisasa wafanyabiashara wa Kinyasini pindi akichaguliwa kushika nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika 29 Oktoba 2025.
Akizungumza na wafanyabiashara na wajasiriamali wa Kinyasini, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Dkt. Mwinyi alisema hiyo ni ahadi yake kwao na alifanya hivyo ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kampeni za chama hicho.
Dkt. Mwinyi pia aliendelea na kampeni zake kwa kuzungumza na kusikiliza changamoto za vijana na wajasiriamali wa sekta ya utalii wa Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja na amewahakikishia kuwa serikali inalenga kuimarisha sekta ya utalii ili kuwanufaisha wananchi wengi zaidi kupitia Sera ya Utalii kwa Wote.



No comments:
Post a Comment