HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 19, 2025

Dkt. Mwinyi: Tudumishe amani

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Mgombea wa Urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Menyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesisitiza suala la amani wakati wa mkutano wa kampeni wa chama hicho kumnadi mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, uliofanyika viwanja vya michezo, Nungwi mkoa wa Unguja, Kaskazini 18 Septemba 2025.

Akizungumza katika mkutano huo, Dkt. Mwinyi alisema wananchi wanapaswa kuendeleza na kudumisha amani kwani ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa letu.

Alisema wananchi wana kila sababu ya kuendelea kuiamini CCM, kutokana na utekelezaji wa kina wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020–2025, ambayo imeleta mageuzi makubwa katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

"Ninawahimiza wana-CCM na wananchi wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025, kushiriki uchaguzi na kuipigia kura CCM ili tuendelee kuimarisha amani, mshikamano na maendeleo ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla" alisema.

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alisema kuwa Dkt. Mwinyi ni kiongozi sahihi, mchapakazi, msikivu na hodari, aliye tayari kupewa kipindi cha pili cha kuiongoza Zanzibar kwa kasi zaidi ya maendeleo.


No comments:

Post a Comment

Pages