HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 19, 2025

HT: Wiliete SC 0-1 Yanga

BAO la kiungo mkabaji Azizi Andabwile, limewapeleka mabingwa wa Tanzania, Yanga mapumziko na uongozi wa 1-0 dhidi ya wenyeji wao Wiliete SC ya Angola.

‎Yanga wako ugenini kwenye dimba la Novemba 11 (11 de Novembro), wakiwavaa Wiliete SC katika mechi ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL 2025/26).

‎Andabwile alifunga bao hilo kunako dakika ya 30, baada ya kupora mpira na kufumua mkwaju wa zaidi ya mita 25, na kumtumgua kila wa Wiliete SC, ambaye kwa dakika 45 za kwanza amekuwa nyota wa mchezo, alifanya 'saves' kubwa zaidi ya tatu kutoka kwa Prince Dube.

‎Hii ni mechi ya kwanza raundi ya awali, ambapo zitarudiana Septemba 27 kwa Yanga wanaonokewa na Romain Folz kuwaalika Wiliete SC ya Bruno Ferry kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.


 

No comments:

Post a Comment

Pages