HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 17, 2025

Dkt. Mwinyi: Wafugaji, wakulima Uzini pigieni CCM

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Wakulima, wafugaji na wananchi eneo la Uzini, wametakiwa wajitokeze kwa wingi ili kuipigia kura CCM ili kuiendeleza Zanzibar kwa kasi zaidi.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni za chama hicho uliofanyika katika uwanja wa michezo Uzini, Wilaya ya Kati, Unguja alisema CCM kitaendelea kuweka mkazo zaidi katika kuwasaidia wakulima na wafugaji ili kuimarisha uzalishaji na kuinua maisha ya wananchi.

"Tutaongeza fungu la bajeti kwa makundi ya wakulima na wafugaji" alisema.

Alisema Dkt. Mwinyi serikali itawapatia pembejeo, mbegu bora, mbolea na masoko ya bidhaa zao kwa wakati.

Alibainisha kuwa mikopo nafuu isiyo na riba kuendeleza shughuli itaendelea kutolewa.


 

No comments:

Post a Comment

Pages