RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ameelezea masikitiko yake kutokana na vifo vya Masista wanne wa Shirika la Masista Wakarmeli Wamisionari wa Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu pamoja na dereva wao, waliofariki kwa ajali ya gari katika eneo la Bukumbi, jijini Mwanza.
Katika taarifa yake, Rais Samia ametuma salamu za pole kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Wolfgang Pisa, Jumuiya ya Masista wa Shirika la Masista Wakarmeli Wamisionari wa Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu, waumini wote wa Kanisa Katoliki na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda.
"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya Masista wanne wa Shirika la Masista Wakarmeli Wamisionari wa Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu pamoja na dereva wao, katika ajali ya barabarani iliyotokea jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo.
"Ninawaombea kwa Mwenyenzi Mungu wapumzike kwa amani na amjalie uponyaji wa haraka mmoja anayeendelea na matibabu.
"Ninatoa salamu za pole kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Wolfgang Pisa, Jumuiya ya Masista wa Shirika la Masista Wakarmeli Wamisionari wa Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu, waumini wote wa Kanisa Katoliki, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa Said Mtanda, ndugu, jamaa na marafiki na wananchi wote kwa msiba huu," imeeleza taarifa ya Rais Samia.
Taarifa kutoka kwa Uongozi wa Jimbo Kuu Katoliki, Mwanza, zinaeleza kuwa gari waliyokuwa wakisafiria iligongana uso kwa uso na lori majira ya saa 5 usiku wa kuamkia jana, wakiwa kuelekea Uwanja wa Ndege, tayari kwa safari ya Dar es Salaam.
Imeeleza kuwa, waliofariki katika ajali hiyo ni: Sista Nerina Simeon raia wa Italia mwenyenumri wa miaka 60, ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Shirika hilo na Sista Lilian Kapongo, Mama Mkuu wa Shirika mwenye umri wa miaka 55.
Wengine ni Sista Damaris Matheka, aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Bukumbi na Sista Stellamaris Muthini, ambaye alikuwa mtawa raia wa Kenya, pamoja na dereva wa gari yao aliyetambulika kwa majina ya Boniface Msonola.
Imeelezwa kuwa, Sista aliyenusurika katika ajali hiyo ni Sista Pauline Mipata mwenye umri wa miaka 20, ambaye ni Matron wa Shule ya Wasichana Bukumbi, ambaye hata hivyo amejeruhiwa vibaya na kwa sasa yupo Chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalum katika Hospitali ya Bugando.
September 17, 2025
Home
Unlabelled
Masista waliokufa ajalini Mwanza hawa hapa, Rais Samia awalilia
Masista waliokufa ajalini Mwanza hawa hapa, Rais Samia awalilia
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.



No comments:
Post a Comment