HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 29, 2025

NMB YAKABIDHI VIFAA TIBA KIGAMBONI

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Dalmia Mikaya leo September 26,2025 amepokea vifaa tiba vilivyotolewa na benki ya NMB ikiwa ni sehemu ya benki hiyo kurudisha sehemu ya faida yake katika Jamii.

DC Dalmia amesema vifaa vilivyotolewa ni pamoja na vitanda vya Wanawake kujifungulia na vitanda vya uchunguzi 20 pamoja na mashine 20 za kusaidia kupumulia kwa Watoto wadogo wenye changamoto.

DC Dalmia ameishukuru NMB kwa kutoa msaada huo ukiwa na lengo la kusaidia mahitaji mbalimbali ya upatikanaji wa vifaa tiba na kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya iliyofanya ya ujenzi wa Hospitali ambayo imekua msaada mkubwa kwa Jamii.







No comments:

Post a Comment

Pages