Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Tanzania
Labour Party (TLP), Yustas Mbatina Rwamugira, ameahidi kubadilisha mfumo
wa kiutawala na kiuchumi nchini endapo atapata ridhaa ya Watanzania
kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 huku akiisifu Tume Huru ya Taifa
ya Uchaguzi (INEC).
Rwamugira
amebainisha hayo akihutubia mkutano wa uzinduzi kampeni uliofanyika Se
katika Viwanja vya Bakhresa, Manzese, jijini Dar es Salaam ambapo
amesema Serikali yake itajikita katika kusimamia utawala bora, uchumi
imara na ajira kwa vijana.
Amebainisha
kuwa mpango wake ni kuhakikisha hospitali zinakuwa huru dhidi ya madeni
sugu yanayokwamisha utoaji wa huduma, pamoja na kuweka mikopo rafiki
inayoweza kufikiwa na wananchi wa kada zote.
Vilevile, ametoa wito kwa wananchi kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu.
Katika
hatua nyingine mgombea huyo, akiwa sambamba na mgombea mwenza wake
Amana Suleiman Mzee, amewaeleza wananchi dhamira ya TLP kuhakikisha kila
Mtanzania anapata milo mitatu kwa siku endapo watachaguliwa kuunda
serikali.
Amesema
azma hiyo ni sehemu ya mikakati ya chama hicho kupunguza changamoto za
kiuchumi na kuinua hali ya maisha ya wananchi, huku akiwataka Watanzania
kuipa kura TLP ili iweze kutekeleza sera zake kwa vitendo.



No comments:
Post a Comment