HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 05, 2025

Dkt. Mwinyi: Tumbatu zinajengwa barabara za zege



Na Mwandishi Wetu, Zanzibar


Mtandao wa barabara katika visiwa vya Tumbatu, utakuwa wa zege kutokana na hali ya ekolojia ya sehemu hiyo.

Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM ambaye pia ni Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi alisema mkandarasi yupo hatua za mwisho kwani ilionekana kitaalam lami isingefaa.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika, Tumbatu Uvivin, Dkt. Mwinyi alisema barabara hizo ni ahadi yake kwao.

Upande mwingine Dkt. Mwinyi ameahidi pamoja na mambo mengine ya maendeleo aliyokusudia kuyafanya pindi akipata ridhaa ya kuiongoza tena Zanzibar ni kuipandisha Tumbatu na kuifanya wilaya kamili.

Alisema Dkt. Mwinyi alisema msingi uliopo katika sera ya Ilani ya CCM ni kudumisha amani, umoja, mshikamano na kuondoa ubaguzi na kama wanataka maendeleo wachague CCM.

Aliwataka wasiwasikilize ambao hawana sera isipokuwa ubaguzi miongoni mwa waZanzibar

No comments:

Post a Comment

Pages