HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 14, 2025

CRDB yazindua huduma Mpya ya Tokenization

BENKI ya CRDB imezindua huduma mpya ya kidijitali inayojulikana kama Tokenization ambayo itawawezesha wale wasiokuwa na akaunti ya benki kupokea fedha kutoka kwa mawakala wa CRDB bila kutozwa gharama ya ziada.

Akizungumza wakati wa kongamano la kuwajengea uwezo katika huduma za uwakala na matumizi sahihi ya mashine za POS, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Muhimuliza Buberwa, alisema kuwa huduma hiyo  mpya ya kidijitali inalenga kuongeza ujumuishi wa kifedha kwa kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za kifedha bila kujali kama ana akaunti ya benki au la.

"Mteja anaweza kutuma au kupokea fedha kwa urahisi kupitia mawakala wetu bila kulazimika kuwa na akaunti. Hii ni njia salama, ya haraka na rafiki,” alisema Buberwa." 

Mkuu wa Kitengo cha Mawakala na Huduma za Malipo wa CRDB, Catherine Lutenge, amesema kuwa semina hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kuwawezesha mawakala kutoa huduma kwa ufanisi zaidi kupitia mafunzo ya matumizi ya mashine za POS na teknolojia mpya ikiwemo Tokenization. 

Kongamano hilo lililowakutanisha zaidi ya mawaka 800 litafanyika pia katika wilaya zingine za Mkoa wa Dar es salaam.


No comments:

Post a Comment

Pages