NA DENIS MLOWE, IRINGA
Chuo
Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE), kikiwa chini ya Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM), kimepongeza juhudi kubwa za Serikali ya Awamu ya Sita
inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji
mkubwa katika sekta ya elimu, kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi
ya Kiuchumi (Higher Education for Economic Transformation – HEET
Project).
Katika taarifa iliyotolewa Rasi wa
Chuo Kishiriki cha Mkwawa, Profesa Method Semiono ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya kumbukizi ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere amesema kuwa mradi huo ni matokeo ya dhamira ya Serikali ya
kuendeleza elimu ya juu ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi nchini.
Alisema
kuwa mradi wa wa HEET ambao serikali ya Rais Samia umekuwa na
Uwekezaji wa Kimkakati katika elimu nchini ikiwa unatekelezwa kwa miaka
mitano (2021/2022–2025/2026) unafadhiliwa na Benki ya Dunia na unalenga
kuboresha ubora wa elimu ya juu nchini.
Profesa
Semioni alisema kuwa kupitia mradi huo MUCE imetengewa kiasi cha Dola
za Kimarekani milioni 8 (sawa na Shilingi Bilioni 18.6 kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati.
Alisema
kuwa Fedha hizo zinatumika katika maeneo sita muhimu: ikiwemo
Uboreshaji wa mitaala na mbinu za ufundishaji, Ujenzi wa miundombinu ya
kisasa , Kuendeleza rasilimali watu kuimarisha elimu jumuishi na usawa
wa kijinsia na Kuboresha matumizi ya TEHAMA na majukwaa ya kidijitali na
Kuimarisha uhusiano kati ya vyuo na sekta binafsi.
Profesa
Semiono alisema kuwa uboreshaji wa Mitaala na Ubunifu katika Elimu
kupitia HEET, MUCE imefanya mapitio ya mitaala mitano ya zamani na
kuanzisha mitaala mipya 30 inayolenga kuongeza ujuzi unaokidhi mahitaji
ya soko la ajira.
Aidha, Chuo kimeanzisha
programu saba za Umahiri (Masters) na mbili za Uzamivu (PhD), na hivyo
kufikisha jumla ya programu 14 za uzamivu kutoka tano (5) za awali hii
katika awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hatua
hii imeongeza fursa za udahili, ambapo idadi ya wanafunzi inatarajiwa
kufikia 10,000. Mitaala mipya inajikita katika kukuza ubunifu, elimu ya
fedha, akili mnemba, na ujuzi wa msingi (soft skills) unaowezesha
wahitimu kujiajiri au kuajirika.
Vilevile
Ujenzi wa Miundombinu ya Kisasa katika kuboresha mazingira ya
kujifunzia, MUCE imetengewa zaidi ya Shilingi Bilioni 15.29 kwa ajili ya
ujenzi wa majengo manne makubwa ambayo ni jengo la Hosteli za Wanafunzi
lenye ghorofa mbili na vyumba vya kusomea, jengo la Maabara ya Fizikia
lenye kituo cha hali ya hewa jengo la Midia Anuwai na Elimu Maalumu
lenye miundombinu ya wanafunzi wenye ulemavu na Jengo la Sayansi
litakalokuwa kituo kikuu cha mafunzo na tafiti za sayansi lenye maabara
za kisasa.
Aidha alisema kuwa
Serikali imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 15 nyingine kwa ajili ya
miradi mingine ya maendeleo, na kufanya jumla ya fedha zilizotolewa kwa
miundombinu ya MUCE kufikia zaidi ya Shilingi Bilioni 30.
Miundombinu
hiyo itasaidia kuongeza udahili wa wanafunzi kwa zaidi ya elfu nne na
kupunguza changamoto ya upungufu wa hosteli kwa wanafunzi wanaoishi nje
ya kampasi.
Mageuzi ya TEHAMA na Ufundishaji wa Kidijitali
Katika
nyanja ya TEHAMA, MUCE inatekeleza ukarabati mkubwa wa mifumo ya
teknolojia ya mawasiliano na kutandaza nyaya za fibre kwa ajili ya
mtandao wa intaneti wa kasi. Ujazo wa intaneti umeongezwa, na majukwaa
ya ufundishaji kwa njia ya mtandao yameanzishwa.
Kwa
hatua hii, wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi
wanaweza kupata elimu ya juu kupitia mfumo wa kidijitali, bila
kulazimika kufika chuoni.
Alimalizia kusema
kuwa kupitia mradi wa HEET, Serikali ya Awamu ya Sita imefanikisha
mageuzi makubwa katika elimu ya juu nchini uwekezaji huu katika MUCE ni
kielelezo cha dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendeleza
elimu bora, jumuishi na yenye tija kwa maendeleo ya taifa.
Alitoa
wito kwa jamii kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29 kwa Dkt
Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya miradi mbalimbali amhayo imeleta na
italeta tija kwa nchi.
Kwa upande wake Rais wa
Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa, Musa Mgema
alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu
Hassan kwa kufanikisha miradi ya makazi wa wanafunzi katika chuo hicho.
Alisema
kuwa ujenzi wa hostell kwa ajili ya wanafunzi itasaidia usalama kwa
wanafunzi na kuwaweka sehelmu salama ambapo awali wengi walikuwa
wanaishi nje ya chuo na kuongeza kuwa ujenzi huo utasaidia kupata
mazingira bora ya kusomea.






No comments:
Post a Comment