HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 05, 2025

Mbeto: Dk Mwinyi ni ramani ya Maendeleo Z'bar

Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimemtaja mgombea wake wa Urais Zanzibar Rais Dkt. Huseein  Ali Mwinyi  miaka mitano iliopita amekuwa dira na ramani iliofikisha Zanzibar katika  uwanja mpana wa maendeleo. 

Pia chama hicho, kimesifu juhudi na  utendaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)  na jina la Dkt. Mwinyi limeingia  katika rekodi ya utumishi uliotukuka.

Matamshi hayo  yametamkwa na Katibu wa Kamati  Maalum ya NEC  Zanzibar, Idara ya Itikadi,mUenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis  alisema Zanzibar ya Mwaka 2025 kimaendeleo si   ya mwaka 2020.

Mbeto alisifu utendaji wa pamoja wa SMZ  na kuitaja miradi mikubwa ya kisekta ilioanzishwa na kukamilika, hivyo maendeleo  yaliopatikana yatabaki kuwa alama isiofutika.

Alisema kutokana na utendaji wa serikali ya awamu ya nane ya Rais Dkt. Mwinyi amefuata nyayo na urithi na matunda ya watangulizi wake katika kusimamia maendeleo ya nchi na watu.

" Rais Dkt. Mwinyi atabaki kuwa mfano na kielelezo cha utumishi bora. Miaka mitano ya serikali yake ametimiza wajibu  kwa wananchi na kufanya mageuzi  makubwa katika ustawi wa jamii" alisema Mbeto.

Katibu huyo Mwenezi alisema licha ya uongozi wa Rais Dkt. Mwinyi kuwa kama dira na ramani iliofikisha mbali Zanzibar kimaendeleo lakini pia wananchi waishi kwa upendo na umoja.

 "Serikali  ya awamu ya nane  Zanzibar  imekomesha maonevu,  ubaguzi na upendeleo. Rais  Dk Mwinyi amekataa kuongoza kwa  visasi na chuki Serikali yake imewajibika na kutumikia wananchi" asisitiza.

Pia Mbeto  alisema  hakuna jambo lolote  litakalomzuia asirudi tena ikulu,  kwani   alioyaahidi  ameyatekeleza ikiwemo kuondosha changamoto alizozikuta  na kufanikisha miradi ya kisekta.

"Wananchi  ili kumtuza Rais Dk Mwinyi wameahidi kumpigia kura nyingi ili akamilishe kazi alioianza mwaka 2020. Mgombea Urais wa CCM  hana deni kwa wananchi wake" alisema Mbeto.


 

No comments:

Post a Comment

Pages