HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

April 04, 2026

Vijana wametakiwa kuchangamkia fursa za mikopo zinazotolewa na serikali ili kujikwamua kiuchumi

NA EDITHA WILLIAM, BUKOBA


Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Bukoba Mjini, Comrade James Michael Nyamanza ambapo  amesema kuwa fursa hizo zinatolewa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mh. Dkt, Samia Suluhu Hassan lengo likiwa ni kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.


Amebainisha kuwa mikopo hiyo inapatikana katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, mifugo, uvuvi, michezo pamoja na nyanja nyingine za kiuchumi, na kusisitiza umuhimu wa vijana kuitumia ipasavyo ili kuboresha maisha yao.


Pia amewahimiza vijana kuwasiliana na maafisa maendeleo ya jamii waliopo katika maeneo yao, ambao wako tayari kutoa msaada wa namna ya kupata taarifa sahihi, kuandaa maandiko ya miradi pamoja na hatua zote muhimu za kufanikisha maombi ya mikopo hiyo.


Aidha, Nyamanza amewakumbusha vijana kutokupuuzia fursa hizo pindi zinapojitokeza, bali wajitokeze kwa wingi kuomba na kunufaika nazo.

No comments:

Post a Comment

Pages