Benki ya CRDB imeandika historia kwa kufanikiwa kupata faida ya shilingi trilioni moja kabla ya kodi katika kipindi cha mwaka uliopita, ikiwa ni hatua kubwa ya mafanikio tangu kuanzishwa kwa benki hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za CEO Awards, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Abdulmajid Nsekela, alisema mafanikio hayo yametokana na juhudi za pamoja za wafanyakazi pamoja na utekelezaji mzuri wa mikakati ya kibiashara.
Alisema tuzo hizo zinalenga kutambua na kuhamasisha wafanyakazi na vitengo vilivyofanya vizuri zaidi ndani ya mwaka uliopita, jambo linalochochea ari ya utendaji kazi bora ndani ya taasisi hiyo.
Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Super Dome uliopo Masaki, ambapo viongozi mbalimbali na wafanyakazi wa benki hiyo walihudhuria.




No comments:
Post a Comment