HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

April 22, 2026

CRDB Yatwaa Tuzo ya Kimataifa ya Huduma za Private Banking

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


BENKI ya CRDB imepata heshima ya kutambuliwa kimataifa baada ya kushinda tuzo ya benki bora katika utoaji wa huduma za kifedha kwa wateja maalum (Private Banking) kutoka taasisi ya Euromoney.



Tuzo hiyo imetolewa Aprili 21, 2026 jijini Dar es Salaam, ikiwa ni hatua inayoonyesha ukuaji wa sekta ya fedha nchini Tanzania na kuimarika kwa huduma za kifedha.


Akizungumza wakati wa kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. AbdulMajid Nsekela, alisema ushindi huo unaweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kuaminika zaidi kimataifa.




Alisema mafanikio hayo yataongeza imani kwa wawekezaji wa ndani na nje, hali itakayochochea ukuaji wa uwekezaji nchini.



“Tuzo hii inaonyesha uimara wa mifumo ya kifedha nchini, hali inayochochea wawekezaji wengi zaidi kuichagua Tanzania kama sehemu salama ya kuwekeza na kuhifadhi mitaji yao,” alisema Dk. Nsekela.



Aidha, alieleza kuwa mafanikio hayo yametokana na usimamizi madhubuti wa sekta ya fedha unaofanywa kwa ushirikiano kati ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Wizara ya Fedha Tanzania, ambazo zimeweka sera rafiki zinazokuza ubora wa huduma za kifedha.



Aliongeza kuwa maendeleo ya teknolojia ya kifedha yameongeza urahisi kwa wananchi na wafanyabiashara kutumia huduma za benki bila kubeba fedha taslimu, jambo linalochangia kuimarika kwa usalama na ufanisi wa miamala.



No comments:

Post a Comment

Pages