Ofisa Michezo BMT, Charles Maguzu (kushoto), akisalimiana na Makamu Mwenyekiti DAA, Mwalimu Elizabeth Tungaraza, alipotembelea Kliniki ya Mazoezi ya Riadha inayoendeshwa na Chama Cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Na Mwandishi Wetu
CHAMA Cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAA), kimeandaa mashindano ya kujipima 'Trial' yanayotarajiwa kufanyika Jumamosi Juni 13 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Hayo yamebainishwa leo Juni 6 na Makamu Mwenyekiti DAA, Mwalimu Elizabeth Tungaraza, mara baada kumalizika kwa Kliniki Maalumu ya mchezo wa Riadha inayofanyika kila Jumamosi kwenye Uwanja huo.
Mwalimu Tungaraza mbali na kuwapongeza vijana, walimu, wazazi na makocha waliojitokeza katika Kliniki ya leo, alibainisha kuwa kuelekea Mashindano ya Taifa yanayotarajiwa kufanyika Julai 3-4 Kibaha mkoani Pwani, wamepanga kufanya majaribio Jumamosi ijayo, ili kuona viwango walivyofikia wachezaji.
Kwa upande wa Kliniki, Leo iliendelea vema chini ya Kocha Mkuu wa Mkoa, Eric Magesa, sambamba na Fred Mhegele, David Mabula na Issa Ismail.
Pia Kliniki ya leo ilipata bahati ya kutembelewa na Ofisa Michezo Mwandamizi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Charles Maguzu, ambaye aliipongeza DAA kwa juhudi zake za kuendeleza mchezo wa Riadha.
"Hongereni sana, nimeona leo nije kuwaona wadau, nawaona mnaendeleza jalamba, hongereni sana tunafarijika tukiona matukio kama haya," alisema Maguzu.
Naye Kocha Magesa, aliwataka vijana kuendeleza utamaduni wa kupenda kufanya mazoezi mara kwa mara, badala ya kusubiri kila Jumamosi.



.jpeg)


No comments:
Post a Comment