HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 04, 2026

CRDB Yawaaga Washindi wa Kampeni ya Tembocard Visa Wanaoelekea Canada

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Benki ya CRDB imewaaga rasmi washindi wa awamu ya kwanza wa kampeni ya "Fainali Ndo Mpango na Tembocard Visa", wanaotarajiwa kuondoka nchini Jumapili, Julai 5, 2026 kuelekea Canada kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia.

Miongoni mwa washindi waliokabidhiwa tiketi zao katika hafla hiyo ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere, ambaye alisema kuwa ushindi wake umetokana na kufanya miamala mingi kwenye maduka pamoja na kufanya malipo kupitia SimBanking.

Akizungumza baada ya kupokea tiketi yake, Makongoro Nyerere aliwahimiza wananchi kuendelea kutumia huduma za kidijitali katika kufanya miamala yao ya kila siku, akieleza kuwa matumizi hayo yanaweza kuwapa nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali kupitia kampeni zinazoendeshwa.



Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi na tiketi za ndege kwa washindi hao, Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Kadi wa Benki ya CRDB, Karington Chahe, alisema kampeni hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na mwitikio mzuri wa wateja waliotumia Tembocard Visa kufanya miamala yao.

"Leo ni siku rasmi ya kuwaaga washindi wetu wa awamu ya kwanza wanaoelekea Canada. Tunawashukuru Watanzania wote, hususan wateja wa Benki ya CRDB na watumiaji wa Tembocard Visa, kwa kuendelea kutumia kadi zao. Matumizi hayo ndiyo yamewaletea fursa ya kujishindia safari hii ya kipekee," alisema Chahe.

Alieleza kuwa washindi hao walihakikisha wanafanya miamala yao yote, iwe ndani au nje ya nchi, kwa kutumia Tembocard Visa, jambo lililowawezesha kushiriki na kushinda katika kampeni hiyo.

Kwa mujibu wa Chahe, kampeni hiyo pia imeongeza matumizi ya huduma za kidijitali, huku ikichangia kupunguza matumizi ya fedha taslimu na hivyo kusaidia kupunguza vitendo vya utapeli na wizi.

Aidha, aliwahimiza Watanzania kuendelea kutumia Tembocard Visa na kuwakaribisha wale ambao hawana kadi au ambazo zimeisha muda wake kutembelea matawi yote ya Benki ya CRDB kwa ajili ya kupata kadi mpya papo hapo.



"Hivi sasa mteja hahitaji tena kusubiri siku saba kama ilivyokuwa awali. Ukifika tawi lolote la Benki ya CRDB unapatiwa Tembocard yako papo hapo na unaondoka nayo," alisisitiza.

Kampeni ya "Fainali Ndo Mpango na Tembocard Visa" ilizinduliwa mwezi Machi 2026 na kufungwa rasmi Juni 11, 2026. Kampeni hiyo iliwahusisha washindi 20, ambapo washindi 10 walijishindia safari za kwenda Canada na Marekani kushuhudia Kombe la Dunia, huku washindi wengine 10 wakijishindia televisheni janja (Smart TV) za inchi 85 pamoja na ving'amuzi.

Lengo la zawadi za televisheni lilikuwa kuwapa fursa wale ambao hawakufanikiwa kushinda safari ya kwenda kushuhudia michuano hiyo moja kwa moja, ili waweze kuifuatilia wakiwa majumbani mwao.

No comments:

Post a Comment

Pages