HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 06, 2026

Vijana Uchumi Challenge 2026 ni jukwaa la kukuza ubunifu na ujasiriamali – Urassa

Mwenyekiti wa CRDB Bank Foundation, CPA (T) Oswald Urassa, amesema programu ya Vijana Uchumi Challenge 2026 imevuka kuwa mashindano ya kawaida na sasa ni jukwaa muhimu la kukuza ubunifu wa kiuchumi, biashara na ujasiriamali kwa vijana nchini.

Urassa amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa fainali za Vijana Uchumi Challenge 2026 na hafla ya utoaji wa tuzo, ambapo alitoa salamu kwa niaba ya mdhamini mkuu wa programu hiyo.

Amesema mafanikio ya programu hiyo yanaonesha nguvu ya ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kuwawezesha vijana kiuchumi. Amefafanua kuwa kuwapatia vijana fursa, elimu na mtaji ni njia muhimu ya kujenga uchumi imara wa Taifa.

“Programu hii imevuka zaidi ya mashindano ya ubunifu wa kiuchumi na biashara. Tumeshuhudia nguvu ya ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kuwawezesha vijana wa Tanzania, na tunaamini kwamba kila kijana anapopewa fursa, elimu na mtaji anakuwa sehemu ya suluhisho la uchumi wa Taifa,” amesema Urassa.

Aidha, Urassa amesema CRDB Bank Foundation itaendelea kushirikiana na Serikali pamoja na wadau mbalimbali katika kuendeleza programu na mipango inayowawezesha vijana kiuchumi, kwa lengo la kukuza ubunifu, ujasiriamali na kuongeza mchango wao katika maendeleo ya taifa.

No comments:

Post a Comment

Pages