HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

October 26, 2026

WANANCHI MLIO UMETOKA

 

 

NA JOHN MARWA 

HATIMAYE, Mlio umetoka, sauti imesikika, mkono umetoka, wino umedondoka, kutoka kwa Wananchi, kamba wameikata iliyokuwa ikiwaunganisha na Kocha Manqoba Mngqithi, baada ya kuona mawimbi ni makubwa lakini joshi halitoshi.
Dakika 1170, sawa na michezo 13, imetosha kuvunja ndoa ya klabu ya Yanga na aliyekuwa Kocha wao Mkuu raia wa Afrika Kusini Manqoba Mngqithi ambaye licha ya kutimuliwa rekodi zake sio haba ukiondoa nama timu imekuwa ikicheza.

Ikumbukwe Kocha Mngqithi alijiunga na Wananchi baada ya msimu wa 2025/26 kumalizika, ambapo hadi anatupiwa vilago ameiongoza Yanga kucheza michezo 13 ya mashindano yote, akishinda 10, sare 3 na kupoteza mmoja.

Katika michezo hiyo 13, Yanga ilifunga mabao 29 huku ikiruhusu mabao 7, ameipeleka timu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAF CL, pia alitwaa Ngao ya Jamii. Je kwa takwimu hizo hazijatosha kumpa Imani zaidi ya kukisuka kikosi chake?

Kumkuwa na muendelezo wa klabu kubwa nchini kutimua Mkocha hata kama ambapo rekodi zao zinawabeba licha ya muda mfupi ambao wanaupata ndani ya timu hizo. Ni kweli ni udhaifu wa Kocha pekee unazifanya klabu hizi kupoteza imani yao ya kucheza ama kuna nini nyuma ya pazia?

Kama kweli Makocha ndio shida, nani anyewaajiri makocha ambao hawana ubora ama falsafa zao hziendani na klabu husika, kwqa sababu hakuna Kocha anajipatia kazi mwenyewe, hivyo kuendelea kufuta kazi walimu ni kichaka cha viongozi wazembe kujifichia?

Utamaduni wa klabu zetu kusajili zaidi ya nusu ya kikosi kila msimu hii, haionekani kuwa changamoto kukosa muda wa kuunda kikosi kazi chenye utambulisho wa klabu. Usajili wa wachezaji ambao hawakizi mahitaji ya timu hili halionekana kuwa tatizo ama ni vipofu wanaongoza vipofu hakuna wakumlaumu bali ni mwendo wa kushikiana magongo?

Klabu zimekuwa na machawa wengi ambao wamefichwa kwenye kichaka cha Wahamasishaji na watu wenye ushawishi ndani ya klabu ambao wamekuwa ‘shangazi kaja’ ya kubebea madhaifu ya viongozi? Nachoka mimi kijana wenu na hizi songombingo za timua timua.

No comments:

Post a Comment

Pages