Viongozi wa Baraza la Sanaa la Taifa wakiwa katika mkutano wa maandalizi ya fainali ya Taifa ya Miss Utalii Tanzania na Bodi ya Miss Utalii Tanzania 2012/2013 zitakazofanyika hivi karibuini
Bodi ya Miss Utalii Tanzania ikiwa katika kikao cha pamoja na Viongozi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
Wajumbe wa Bodi ya Miss Utalii Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
WAKATI kambi ya Miss Utalii Tanzania 2012/2013
ikikaribia kuanza katika Hotel ya Ikondolelo jijini Dar es salaam, juzi tarehe
14.12.2012 Bodi ya Taifa ya mashindano hayo ilifanya kikao na Serikari kupitia
Baraza la Sanaa la Taifa katika ukumbi wa Baraza hilo. Katika kikao hicho
ambacho kilijadili maandalizi ya fainali na mpango mkakati wa fainali za
taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu.
Katika kikao hicho Bodi ya Miss Utalii Tanzania
iliwasilisha taarifa ya kukamilika kwa maandalizi kwa Serikali ambapo bodi
iliitaarifu Serikali kuwa maandalizi ya fainali hizo yamekamilika kwa asilimia
tisini 90% ikiwemo katika maeneo ya kambi na mafunzo, ukumbi, Zawadi,
wadhamini,Washiriki, Nk.
Bodi ilibainisha kuwa kwamba jumla ya washiriki
sitini (60) wakiwakilisha mikoa yote ya Tanzania na Kanda maalum za vyuo vikuu
watapanda jukwaani kuwania taji la Miss Utalii Tanzania 2012/2013. Pia
Bodi ilibainisha kuwa zawadi zitakazo tolewa kwa washindi zimelenga zaidi
kuwanufaisha washiriki , jamii zao na taifa. Zawadi hizo ni pamoja na Nafasi za
masomo za elimu ya juu, mikataba ya kazi ,Safari za kushiriki mashindano ya
Dunia na Kimataifa , Tuzo za heshima za kijamii, kitalii, kitamaduni, urembo na
mitindo.
Aidha Bodi ilielezea kuwa imejipanga kuzifanya
fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/2013 kuwa tukio kubwa la pekee
Kihistoria na kitamaduni kuwahi kufanyika nchini kabla na baada ya uhuru.
Ambapo wakiwa kambini washiriki watafanya shughuli mbalimbali za kijamii
pamoja na kupata mafunzo stadi mbalimbali za maisha , uhamasishaji na
utangazaji wa elimu , utalii, utamaduni, uwekezaji,mazingira, michezo na afya.
Nayo Serikali ilipongeza Bodi ya maandilizi ya
miss utalii Tanzania kwa mpango mkakati na maandalizi yenye kukidhi na kulenga
kupromoti utalii uhamasishaji na utangazaji wa elimu, utamaduni,
uwekezaji,mazingira, michezo na afya.Akizungumza katika mkutano huo Kaimu
Katibu Mtendaji wa Baraza la sanaa la Taifa Ndugu.
Malimi Mashili alipongeza
mpangilio wa zawadi na tuzo kwa washindi pamoja na washiriki ambapo tofauti na
mashindano mengine ambapo zawadi zao huwa ni mzigo kwa washiriki na wakati
mwingine zisizo na manufaa kwa jamii wala Taifa."
Miss utalii
Tanzania katika kipindi cha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake imekuwa
ni fahari ya Taifa na kielelezo cha utamaduni wa Tanzania kitaifa na kimafaifa
ambapo limekuwa ndilo shindano pekee linalo la tangaza nchi yetu kwa kushinda
mataji ya Dunia na kimataifa kila mnapo shiriki".
Aidha akiahirisha
mkutano huo aliihakikishia Bodi kuwa Serikali inatambua juhudi na mchango wa
waandaaji na mashindano ya miss utalii tanzania katika kukuza utalii, utamaduni
na michezo nchini na kwamba Serikali sikuzote ipo bega kwa bega na
waandaaji wa mashindano haya katika kuhakikisha kwamba hayakwami na iko tayari
kusaidia kwa hali na mali ili yaweze kufanyika kwa kiwango cha kimataifa.
Imetolewa na,
Mratibu Matukio,
Hamis .A. Mkongowale
No comments:
Post a Comment